Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Sayansi na Technolojia (VIST) imeahidi kuwanoa maofisa tabibu wenye weledi ili kuongeza nguvu jitihada za serikali za kuwekeza kwenye sekta ya afya.
TAASISI ya Sayansi na Technolojia (VIST) imeahidi kuwanoa maofisa tabibu wenye weledi ili kuongeza nguvu jitihada za serikali za kuwekeza kwenye sekta ya afya.
Kimesema serikali ya awamu ya tano imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya afya hivyo wadau binafsi wanawajibika nao kuweka nguvu zao ili kuongeza wataalamu wengi kwenye sekta ya afya.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Naidu Katuri wakati akizungumzia uzinduzi wa chuo hicho kilichopo Mbezi Beach mkabala na kiwanda cha Interchick barabara ya Bagamoyo jijini Darves salaam.
Katuri amesema kwa kuwa kuna uhaba wa watumishi wa sekta ya afya hususan maofisa tatibu taasisi hiyo imejipanga vya kutosha kuhakikisha kinazalisha wataalamu hao wengi na wenye sifa zinazotakiwa.
Amesema taasisi yake imegundua kuwa wataalamu hao wanahitajika kwa wingi hasa maeneo ya vijijini ambako ndiko idadi kubwa ya watanzania iliko.
Katuri ameongeza kusema kuwa taasisi hiyo imejidhatiti kufanikisha maono ya mwaka 2025 ya mkakati wa kitaifa wa kukukuza uchumi na kuondoa umaskini nchini.
"VIST itatumia wahadhiri wake wenye uzoefu wa kutosha na vifaa vya kisasa vya kufundishia kuhakikisha tunatoa wataalamu walioiva ambao watakwenda kufanya kazi kwa maadili na weledi", amesema Katuri.
“Tumeshapewa Baraka na Baraza la Taifa Ithibati (NACTE) na limeanza kupokea maombi ya wanaotaka kujiunga na stashahada ya tiba ya (NTA Level 4-6) kwa mwaka wa masomo wa 2020-21,” amesema.
Aidha ameongeza kuwa mwanafunzi atakayetaka kujiunga na taasisi hiyo awe na ufaulu wa alama D kwenye masomo ya Kemia, Biolojia, na Fizikia katika masomo ya kidato cha nne na pia wanatarajia kupanua kwa kutoa program nyingi zaidi mwaka ujao wa masomo katika fani za sayansi na teknolojia kama famasia, teknolojia, maabara, uuguzi na mifumo ya taarifa,” alisema Katuri.
Pia amesema wanatarajia kwa kuanza wawe na wanafunzi 150 wa stashahada ya tiba na mpaka kufikia mwaka ujao wa masomo wawe na wanafunzi zaidi ya 1,000 kwenye fani mbalimbali.
“Tunaomba wazazi na walezi watuamini watuletee wanafunzi wao maana watapata kile wanachotaka na wanaopenda watembelee ofisini kwetu au kwenye webu yetu ya websitewww.vist.ac.tz,” amesema Katuri.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vist, Naidu Katuri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...