Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia , Profesa James Mdoe akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ulinzi na usalama katika utumishi wa umma kwa watumishi wa kada ya walinzi yanayofanyika kwa muda wa siku 10 kunzia Juni 15, mwaka huu (2020) katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Savoy -Manispaa ya Morogoro na ( wa kwanza kushoto) ni Mratibu wa Mafunzo na Mkufunzi mkuu kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA),Dk Hassanal Issaya (kwanza kulia) ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Dk Momole Kasambala.

Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma , Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu , Dk Momole Kasambala akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kada ya ulinzi na Usalama wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia uliofanyika mjini Morogoro.
Picha mbalimbali katika Mkutano wa mafunzo ya ulinzi na Usalama katika utumishi wa Umma yalifanyika mjini Morogoro.
Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia , Profesa James Mdoe akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya ulinzi na usalama katika utumishi wa umma kwa watumishi wa kada ya walinzi yanayofanyika kwa muda wa siku 10 kunzia Juni 15, mwaka huu (2020) mjini Morogoro.
Na Mwandishi wetu , Morogoro
WIZARA ya Elimu , Sayansi na Teknolojia umeamua kuendesha mafunzo ya ulinzi na usalama katika utumishi wa umma kutokana na changamoto na matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza katika utendaji kazi kwa watumishi wa kada ya walinzi.
Kaimu Katibu mkuu wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe ,alisema hayo jana katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya ulinzi na usalama katika utumishi wa umma kwa watumishi wa kada ya walinzi yanayofanyika mjini Morogoro.
Alisema kuwa ,matukio hayo yamekuwa yakisababisha hasara kubwa katika wizara , na miongoni changamoto hizo ni upotevu na wizi wa mali na vifaa vya wizara unaofanywa na baadhi ya walinzi au kwa kushirikiana na watu waovu.
Profesa Mdoe ,alizitaja baadhi ya changamoto hizo mbali na upotevu na wizi wa mali na vifaa pia kada hiyo kujihusisha na vitendo vya ulevi wakati wa kazi, mahudhurio hafifu na wakati mwingine kukosa kufika katika sehemu za kazi bila taarifa au ruhusaa ya wasimamizi wao , kuacha malindo wazi bila ulinzi pamoja na kujojitambua vyema jukumu lao la ulinzi sehemu za kazi.
Kaimu Katibu Mkuu huyo , alisema mienendo na vitendo hivyo vinatoa taswira mbaya kuhusu watumishi wa kada ya walinzi walioajiriwa katika utumishi wa umma , utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa maadili ya utendaji katika utumishi wa umma.
Profesa Mdoe, alisema katika kukabiliana na changamoto hizo, uongozi wa wizara umechukua hatua za makusudi za kuwaadalia mafunzo maalumu ya ulinzi na usalama katika sehemu za kazi.
Alisema ,lengo ni kuwawezesha kupata maarifa na ujuzi ,ili waweze kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao ya ulinzi pamoja na kufanya marekebisho ya mapungufu yanayobainishwa.
Hata hivyo , alisema walinzi wengi wamekuwa wakisahaurika katika kupatiwa elimu na mafunzo ya mara kwa mara na kuwafanya kukosa mbinu za kisasa za ulinzi kukabiliana na hali isiyo salama katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kukosa mawasiliano na wateja,wadau,wananchi na watumishi wengine hali inayosababisha migogoro isiyokuwa ya lazima.
“ Wizara imetumia rasimali fedha na muda katika kufanikisha kufanyika kwa mafunzo haya , uongozi wa wizara uliona ni vyema nanyi mjengewe uwezo ili muweze kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi zaidi “ alisema Profesa Mdoe.
Hata hivyo ,alitumia fursa hiyo kuupongeza Uongozi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA),kwa kupewa jukumu la kuendesha mafunzo ya ulinzi na usalama katika utumishi wa Umma kwa watumizi wa wizara hiyo.
Naye Mratibu wa Mafunzo hayo na mkufunzi mkuu kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA),Dk Hassanal Issaya, alisema watumishi wa kada ya walinzi wapatatiwa mafunzo ya siku 10 kuhusu usalama wa ofisi za serikali, taratibu za ulinzi katika ofisi za seriklali , utimamu na nidhamu kwenye ofisi za serikali.
Dk Issaya , alisema mafunzo hayo yatatolewa na wakufunzi wabobezi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama ni watajifunza kutambua na kuzuia uharifu maofisini , makabidhiano ya malindo sehemu za kazi.
Dk Issaya, alitaja eneo lingine la mafunzo hayo ni namna ya kuishi na mhalifu kabla ya uhalifu haujatokea , ulinzi shirikishi, upekuzi , wajibu wa mlinzi wa utumishi wa umma pamoja na kujifunza masuala ya uhalifu wa kimtandao ambalo kwa sasa ni janga kubwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia , Jonathan Kabengwe , alisema mafunzo hayo ni sehemu ya mpango kazi wa wizara wa mwaka 2019/2020 ambayo yamekuwa watolewawa kada mbalimbali za wizara wakiwemo watumishi hao wa kada ya walinzi .
Kabengwe, alisema katika mafunzo hayo jumla ya watumishi wa kada hiyo 64 watanolewa ambapo 26 kutoka Vyuo vya Ualimu , 30 vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC) na nane kutoka udhibiti ubora wa shule .
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo mwenyekiti wa mafunzo ,Nestory Omune , alisema mara kadhaa walinzi wamekuwa wakisingiziwa kupotea kwa vifaa ama mali za umma ambapo alitolea mfano kwenye vyuo kuwa na tabia ya kuwashtaki walinzi kuhusika na wizi wakati hakuna ukweli wowote.
Alisema walinzi wa maeneo husika wamekuwa hawana mahusiano mazuri mahapa pa kazi huku wakifanyakazi katika mazingira magumu kwa kutojengewa vibanda vya kujikinga na mvua ama jua ikiwa na maeneo kukosa na uzio na kufanya watu wasio waaminifu kutumia njia za panya kupitisha vifaa wanavyoiba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...