Na Zainab  Nyamka

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeachana na Katibu wake Dkt David Ruhago baada ya kufikia makubaliano kwa pande zote mbili.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo wamesema kuwa makubaliano ya kusitisha mkataba wa ajira ya Ukatibu Mkuu ndani ya Yanga yamefikiwa leo Juni 15 mwaka huu.

Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga Hassan Bumbuli imesema kusitishwa kwa ajira hiyo ni baada ya majadiliano ya pande zote mbili kwa maslahi mapana ya Klabu ya Yanga.

Amesema, kufuatia hivyo kuanzia siku ya leo Juni 15 Dkt Ruhago ameachia rasmi nafasi ya Ukatibu Mkuu.

Kamati ya utendaji chini ya Mwenyekiti Dkt Mshindo Msolla amemshukuru kwa utumishi wake ndani ya Klabu ya Yanga katika kipindi chote walichokuwa pamoja.

Aidha, katika kipindi nafasi hiyo itakaimiwa na Mwanasheria Simon Patrick ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria na wanachama hadi pale Katibu Mkuu atakapopatika
na.

Dkt Ruhago ameweza kuihudumu Yanga kwenye  nafasi ya Ukatibu Mkuu kuanzia Novemba 11 2019 baada ya kipindi kirefu toka kujiuzulu kwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa na nafasi hiyo kukaimiwa na viongozi tofauti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...