Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
INAAMINIKA
kuwa chimbuko la kusherekea siku za kumbukizi za kuzaliwa maarufu kama
'Birthday' zilianzia barani Ulaya kabla hata ya kuanza kwa ukristo,
katika imani ya kipagani iliaminika kwamba mapepo huwatembelea watu
katika kumbukizi za siku zao za kuzaliwa, hivyo wakatumia siku za
kuzaliwa kujumuika na ndugu na marafiki ili wasitembelewe na mashetani.
Katika
imani hiyo ya kipagani iliamini imani za kishirikina katika sikukuu za
kuzaliwa, waliamini kwamba mashetani huvutiwa sana na watu katika
sikukuu zao za kuzaliwa "Birthday" kwahiyo watu wenye imani ya kipagani
waliwalinda washerehekewa katika siku zao za kuzaliwa ambapo ndugu na
marafiki waliwatembelea ili kuwakinga na madhara ya mashetani kwa
kuwazunguka, kuwaombea heri pamoja na kupiga kelele kubwa kwa malengo ya
kuwaogopesha na kuwakimbiza mashetani.
Baadaye
ukaja utamaduni wa keki na kuwasha mishumaa ambapo baadhi ya watu
waliamini kwamba utamaduni huo ulianzia kwa wagiriki ambao walitengeneza
keki yenye muundo wa mwezi na kuiweka katika hekalu la Armites (Mungu
wa mwezi) na wengine waliamini utamaduni huo ulianzia kwa wajerumani
ambao walitengeneza mkate ulio na umbo la mtoto Yesu akiwa na nguo za
kitoto.
Kinachofahamika
na wengi zaidi ni kwamba utamaduni wa keki na mishumaa umetokana na
imani ya kidini ambao wengi huamini Mungu anaishi mawinguni na kupitia
mishumaa inayowashwa husaidia kupeleka maombi na ishara kwa Mungu, huku
Wajerumani wakiamini kuweka mshumaa mkubwa katikati ya keki huashiria
"Mwanga wa Maisha."
Utamaduni
wa kusherekea siku za kuzaliwa umeendelea hadi sasa ambapo wengi huweka
heri zao kimoyomoyo pindi wanapozima mishumaa, na huaminika kuzima
mishumaa yote kwa pumzi moja huleta bahati nzuri.
Unaamini nini katika kusherekea siku yako ya kuzaliwa? kula keki na kuzima mishumaa huwa unamaanisha nini?



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...