Na Mwandishi Wetu, Babati

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Mkoani Manyara, wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya JACO Service Group, John Stepheni Kabelinde (Babu Joha) kwa kujipatia isivyo halali kandarasi ya kufyeka nyasi pembeni ya barabara. 

Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo mjini Babati Julai 9 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari. 

Makungu amesema Kabelinde maarufu kwa jina la Babu Joha huonekana mara kwa mara maeneo ya Sinza Makaburini jijini Dar es salaam ambapo inasadikiwa ndipo anapoishi na kuendesha shughuli zake. 

Amesema wanamtafuta Babu Joha kwa sababu anatuhumiwa kujipatia kandarasi inayohusu kufyeka nyasi pembeni mwa barabara inayotoka Babati hadi Gehandu Mkoani Manyara. 

Amesema uchunguzi unaonyesha Babu Joha aliwasilisha nyaraka za kupotosha zilizomuwezesha kuwashinda wazabuni wengine tisa walioomba kazi hiyo. 

Amesema uchunguzi unaonyesha Babu Joha kupitia kampuni yake ya JACO Service Group amekuwa akikwepa kulipa kodi mbalimbali za serikali hivyo kuangukia kwenye makosa ya kuhujumu uchumi wa Taifa. 

"Ni rai yangu kwa wananchi wa mkoa wa Manyara na watanzania wote kupitia kwenu wana habari popote babu Joha atakapoonekana toeni taarifa kwa ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu nanyi au kupitia namba yetu ya dharura ya 113 au kamanda wa TAKUKURU mkoani Manyara 07388150124-25," amesema Makungu. 

Amezionya kamati za tathimini za taasisi za ununuzi kutimiza majukumu yao kwa kuhakiki kila kampuni wanayoifanyia tathimini kuona uhalali wa nyaraka zilizowasilishwa na kujiridhisha iwapo kampuni husika inalipa kodi za Serikali. 

"Kushindwa kufanya hivyo ni matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha k/f cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika," amesema Makungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...