Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Msham Munde (kushoto) ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mkuranga akimkabidhi fomu Mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzu Mapinduzu ,Abdallah ulega Agosti 21, 2020.
Mgombea Ubunge aliyeteuliwa na chama cha mapinduzi jimbo la Mkuranga mkoa wa Pwani,Abdullah Ulega akizungumza na wanachama wa chama Mapinduzi Baada ya kuchukuwa fomu ya kugombea ubunge leo Agosti 21,2020.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
MGOMBEA Ubunge aliyeteuliwa na Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mkuranga Abdalah Hamisi Ulega amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo leo katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilayani Mkuranga mkoani pwani.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo ulega amekishukuru chama cha mapinduzi kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi hiyo.
Amesema walikuwa Wana CCM wengi katika mchakato wa ndani ya chama ili kumpata mmoja hivyo kwasasa wote wanaongea lugha moja ambayo ni ushindi wa chama pekee na kuwasihi wana Ccm wote kuunganisha nguvu zao ili kutafuta ushindi wa kishindo
Hata hivyo amesisitiza kuwa huo ni mchakato wa kidemokrasi na baaada ya kipenga na kampeni kuanza atafika katika vijiji vyote vya mkuranga kuomba ridhaa ya kukichagua chama cha mapinduzi .
Katika safari hiyo ameongozana na viongozi mbali mbali wa chama akiwemo Ally Msikami mwenyekiti na Rukia Mbasha katibu wa chama wilaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...