Na mwandishi wetu, Geita

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko, limeendelea  na kampeni yake ya kutoa  elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa migodi  na wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka safari hii mkoani Geita.

Migodi iliyotembelewa na kikosi kazi hicho cha TANESCO ni pamoja na Migodi ya Geita mjini, Wilaya za  Nyanghwale na Bukombe, lakini pia mashine za posho mills zilizotembelewa ni za Buseresere Kasamwa, Nyanghwale,Bukombe, Katoro na Geita mjini.

Kwa mujibu wa Eng Ally Koya kutoka kitengo cha masoko Tanesco makao makuu alisema lengo hasa la kampeni hiyo ni kuwawezesha kufahamu  jinsi ya kupunguza gharama ambazo si za lazima kwa kununua vifaa vya kisasa  na kuachana na vifaa vilivyochakaa na vya zamani kwani vinatumia umeme mwingi.

Wamiliki hao walielimishwa kuhusu utaraibu wa kufunga motor za kisasa na kuzifanyia service mara kwa Mara ili motor iendelee kuwa na ufanisi.

“Matumizi bora na sahihi ya umeme ni muhimu kwa usalama kwani umeme  ni nzuri kama ukiutumia kwa kuzingatia usalama lakini pia umeme ni moto mara moja.” Alisema Mhandisi………….

Walipewa pia elimu ya kufunga power factor ili iweze kuwasaidia uendeshaji wa mitambo yaani kVA haitakuwa kubwa.

Aidha wamiliki wa migodi na mashine walishukuru ujio wa wataalamu hao wa TANESCO kwani umewaongezea uelewa na hivyo kuongeza ufanisi katika eneo la matumizi sahihi ya nishati hiyo ya umeme.


Wafanyakazi wa mgodi wakipewa elimu ya usalama
Fundi wa mitambo katika mgodi wa m/s AURA Mineral akiwaeleza timu ya Tanesco hatua zote wanazofanya hadi kupata dhahabu,kutoka kulia ni afisa masoko toka Tanesco makao makuu bi Jennifer Mgendi,wa pili ni bi Emma Nyaki afisa uhusiano na huduma kwa wateja mkoa wa Geita na eng Ally koyya kutoka Tanesco makao makuu.

Fundi wa mgodi wa Genge tatu extech alishauriwa anaposuka motor asisuke zaidi ya mara mbili

Afisa uhusiano na huduma kwa wateja mkoa wa Geita akiandika changamoto wanazozipata hapo mashineni

Eng Ally Koyya kutoka kitengo cha masoko akimshauri mmiliki wa masika posho mills jinsi ya kutumia matumizi bora ya umeme

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...