Mwonekano wa vitanda katika wodi ya mama na mtoto ambayo ni miongoni mwa majengo
yaliyojengwa kupitia fedha kwa ajili ya upanuzi wa kituo. Wodi hii ina jumla ya vitanda 18.


HALMASHURI ya Manispaa ya Singida ni mingoni mwa Halmashauri  35 za Tanzania Bara zilizotembelewa na Katibu Mkuu wa wa Jumiya za Mamlaka za serikali za Mitaa ALAT Bw. Elirehema Kaaya kujionea utekelezaji wa  miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Hamashauiri hizo kupitia fedha za Mapato ya Ndani, Serikali Kuu, Wahisani na pia jitihada za jamii.
Bwana Kaaya alisema miradi atakayotembelea ni ile ya Huduma kama vile miradi ya Sekta za Afya ,elimu na barabara ambayo imeonesha mafanikio kwa kiwango kikubwa na imetekelezwa kwa njia shirikishi na kwa kuzingatia  ubora .
“Serikali ya awamu ya tano imejenga jumla ya vituo 352 vipya vya kutolea huduma za afya na vimejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kupitia Force account”, alisema.
Kwa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Bw. Kaaya ameweza kutembelea kituo cha Afya Sokoine ambacho kimepanuliwa kwa kuongeza jumla ya majengo 7. Kituo hiki kilipokea kiasi cha Tsh. 500,000,000/- kwa ajili ya upanuzi huo ambao ulihusisha Majengo 7 ambayo ni Pamoja na ;
  • jengo la upasuaji
  • Wadi ya mama na motto
  • Jengo la Maabara
  • Nyumba ya kuhifadhia maisti
  • Jengo la kufulia
  • Na Kichomea taka
Aidha vifaa kama meza za upasuaji, Taa kwa ajili ya upasuaji, mashine za kutoa dawa za usingizi, majokofu kwa ajili ya kuhifadhia maiti, mashine ya kufulia na ya kunyoosha mashuka na vifaa vya maabara vimenunuliwa kupitia fedha hizo za maboresho ya huduma za afya.
Pamoja na majengo hayo, Halmashauri ya Manispaa kupitia mapato yake ya ndani imeweza kujenga njia za kupita wagonjwa (walkways) kwa gharama ya Tshs. 11,000,000/-; Jengo la mionzi ( X- ray)  ambalo linatarajiwa kutumia Tshs. 56 hadi kukamilika kwake. Kwa sasa limetumia Tshs. 21,000,000/-
Tangu kupanuliwa kwa huduma na majengo katika kituo cha afya Sokoine wagonjwa wameongezeka kwani kwa sasa jumla ya wakina mama 680 hufika kujifunga katika kituo hicho kwa mwezi.
Kituo cha Afya sokoine Pia kilipokea fedha za Ufanisi kupitia Mfuko wa Pamoja (Health Sector Basket Fund  Performance Treche) ambazo zililenga katika kukarabati jengo la wagonjwa wa nje ( OPD), Ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa na wanaotembelea wagonjwa, Ukarabati wa tanki la maji na usimikaji wa taa katika chumba cha upasuaji. Kiasi cha Tshs. 42,000,000/- kilipokelewa  kwa mchanganuo ufuatao:
  • kukarabati jengo la wagonjwa wa nje ( OPD)   Tshs. 19,358,750.00
  • Ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa          Tshs. 11,147,500.00
  • Ukarabati wa tanki la maji           Tshs.   6,336,875.00
  • usimikaji wa taa katika chumba cha upasuaji   Tshs.           5,156,875.00
Majengo yote yamejengwa kupitia force account  yamekamilika na yanatumika.
                             
Aidha  Bw. Elirehema Kaaya aliweza pia kutembelea mradi uliotekelezwa na kukamilika wa Jengo la ofisi ya Udhibiti  Ubora wa Shule, Halmashauri ya Manispaa ya Singida, na kuweza kupatiwa taarifa ya mradi tangu kuanza hadi kukamilika. Pia aliweza kukagua jengo na eneo zima la mradi.
Akitoa maelezo Mdhibiti ubora wa shule Bi. Beatrice Joseph alisema Mradi wa jengo la Ofisi ya udhibiti Ubora wa Shule Pamoja na ununuzi wa samani za ofisi na vitendea kazi umegharimu kiasi cha Tshs 152,035,600 kwa mchanganuo ufuatao: 
  • Jengo limegharimu tsh.           137,777,100.00
  • Ukarabati wa samani 8,062,000.00
  • Utengenezaji wa viti4 na meza 1,396,500.00
  • Vifaa vya ofisi 4,800,000.00
Miundombinu ya Barabara ni miongoni mwa miradi aliyoitembelea Bw. Kaaya ambayo kwa sehemu kubwa imechangia katika kuinua shughuli za kiuchumi na  usalama wa raia kutokana na barabara za mitaa kujengwa kwa kiwango cha lami pia uwepo wa taa za barabarani nyakati za usiku.
“ wananchi katika Manispaa ya Singida wameweza kuongeza kipato kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi lakini pia usalama wa raia kutokana na uwepo wa taa za barabarani, viwanja kuongezeka thamani kutokana na barabara nyingi kupitika” alifafanua Mchumi wa Manispaa Deus Luziga
Halmashauri ya Manispaa ya Singida imeweza kujenga barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 9.15 katika awamu mbili za utekelezaji.
Awamu ya kwanza ya ujenzi ilitekelezwa mwaka 2016 ambapo barabara zenye urefu wa 2.65 km zimejengwa kwa gharama ya Tshs. 6,156.916,536.11 wakati awamu ya pili ilitekelezwa 2017/2018 kwa kujenga barabara zenye urefu wa 6.5 km kwa  gharama ya Tshs. 10,529,171,221.95  sambamba na uwekaji wa taa za barabarani zote kupitia mradi wa uboreshaji miji ( LGSP)
Bw. Elirehema Kaaya alihitimisha ziara yake kwa kupongeza Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kazi nzuri ambayo ni matokeo ya usimamizi shirikishi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“ Im so much impressed kwa kazi iliyofanyika, majengo mazuri na huduma za afya ni bora, barabara nzuri  Nimejionea mwenyewe fedha za Serikali zilivyo fanya kazi majengo ya kituo cha afya ,jengo la Mdhibiti Ubora Elimu na barabara yamejengwa kwa ubora wa hali ya juu thamani ya fedha inaonekana nampongeza Mkurugenzi kwa kazi nzuri ya kusimamia fedha za serikali “” alihitimisha Katibu Mkuu wa ALAT, Bw Kaaya.

Picha

  1. Mkurugenzi wa Manispaa Bravo K. Lyapembile akitoa maelezo ya awali kuhusiana na Miradi ya Maendeleo kwa Katibu Mkuu wa Jumiya za Serikaliza Mitaa Bw. Elirehema Kaaya, Pembeni kulia ni Mchumi wa Manispaa ya Singida Deus Luziga.
  2. Mganga Mfawidhi wa Kitu cha Afya Sokoine Dr. Maisara Karume akimtembeza Katibu Mkuu ALAT katika jengo la upasuaji kituoni hapo.
  3. Mganga mfawidhi  Dr. Karume akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa njia za kupitisha wagonjwa ( Walk ways) zilizojengwa kupitia mapato ya ndani ya Manispaa
  4. Moja ya njia za wagonjwa zilizojengwa kutoka chumba cha upasuaji kuelekea wodini
  5. Katibu Mkuu ALAT akikagua mjia za kupitisha wagonjwa
  6. Dr. Karume Akimwongoza Bw. Kaaya kukagua wodi ya mama na mtoto

  1. Bw. Elirehema Kaaya akiongea na mmoja wa kina mama aliyejifungua katika kituo cha Afya Sokoine
  2. Mwonekano wa vitanda katika wodi ya mama na motto ambayo ni miongoni mwa majengo yaliyojengwa kupitia fedha kwa ajili ya upanuzi wa kituo. Wodi hii ina jumla ya vitanda 18.
  3. Bw. Kaaya akikagua mashine katika jengo la kufulia nguo ( Loundry)
  4. Dr. Karume akimwonesha Bw. Kaaya Jokofu la kisasa lenye uwezo wa kuhifadhi miili/ maiti sita
  5. Mwonekano wa Jengo la mionzi ( x-ray) ambalo linajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa
  6. Mtumishi wa Maabara akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa ALAT Bw. Kaaya
  7. Jengo la kupumzikia wagonjwa  lililojengwa kupitia fedha za ufanisi za Mfuko wa Pamoja
  8. Kichomea taka za hopitali ni miongoni wa majengo 7 yaliyojengwa kwa fedha kutoka serikali kuu
  9. Seksheni ya Huduma za dawa katika Kituo cha afya Sokoine ikiwa ni sehemu ya maboresho ya huduma 
  10. Mwonekano wa Jengo la Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule Halmashauri ya Manispaa ya Singida
  11. Mdhibiti Ubora wa Shule Bi. Beatrice Joseph akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu ALAT Bw. Elirehema Kaaya na Mchumi wa Manispaa Singida Bw. Deus Luziga 
  12. Mwonekano wa chumba cha Mikutano katika Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Singida.
  1. Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Lyapembile akiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya serikali za Mitaa ( ALAT)Bw.  Elirehema Kaaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...