Na Woinde Shizza, Michuzi TV, ARUSHA
VIONGOZI wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha usafiri wa Treni unafiki katika Mkoa wa Arusha kwa usalama.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta, alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa tawala, Maafisa Tarafa na wenyeviti wa halmashauri ya jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru.

Alisema maono ya Rais ni kuhakikisha Treni inafika Arusha mwishoni mwa mwezi Agosti ili isaidie sekta ya usafirishaji na kuokoa muda wa wananchi kusafiri muda mrefu.

Ni miaka 30 imepita tangu Treni ifike Mkoani Arusha, hivyo wananchi tunatakiwa kufurai na kuipokea kwa moyo mkunjufu.

Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa ajali kutoka shirika la Reli Tanzania Maizo Mgedzi alisema, wananchi wanatakiwa kuchukua taadhari hasa kipindi ambacho treni itaanza kufanya kazi hasa wanaofanya shughuli mbalimbali karibu na reli.

Alisema ni hatari sana kufanya shughuli mbalimbali za kibinadamu karibu na Reli kama kulima, kupitisha Wanyama, kuegesha Pikipiki na Magari,kuwa na Viwanja au kujenga karibu na reli.

Treni inaenda kuwa msaada mkubwa sana kwani itakuwa inaleta marighafi mbalimbali kwa ajili ya viwanda vilivyopo Arusha na hata kwa wafanyabiashara.

Mkoa wa Arusha kwa mara nyingine tena inaenda kuanzisha safari zake za Treni kutoka Mkoa wa Dar es Salaama hadi Arusha baada ya usafiri huo kusimama takribani miaka 30 sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta, akizungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa tawala, Maafisa Tarafa na wenyeviti wa halmashauri ya jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru katika ukumbi wa mikutano wa jengo la halmashauri ya Meru.
(Picha na Woinde Shizza)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...