
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI Mkuu wa Japan Shinzo Abe ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiafya ndizo zilizopelekea kuchukua maamuzi hayo.
"Ninaomba radhi kwa watu wa Japan."
Ni sehemu ya ujumbe uliotolewa na Shinzo na kueleza kuwa hataki ugonjwa wake kuwa sehemu ya kufanya maamuzi na amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kwa kushindwa kumaliza msimu wa uongozi uliokuwa ukimalizika mwaka 2021.
Shinzo (65) tangu ujana wake amekuwa akiugua ugonjwa wa vidonda na uvimbe kwenye utumbo mpana na hali yake imeendelea kuwa mbaya kwa nyakati za karibuni.
Mwaka uliopita Shinzo alikuwa waziri mkuu mkongwe zaidi nchini humo tangu alipoanza kuitumikia ofisi mwaka 2012.
Aidha, Shinzo atabaki katika nafasi yake hadi pale mrithi wake atakapoteuliwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...