Na Woinde Shiza, Michuzi Tv ARUSHA
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Tundu Lissu pamoja na Mgombea Mwenza wake Salim Mwalimu wanatarajia kuingia mkoani Arusha Agosti 14 ,2020 mkwa ajili yakusaka wadhamini katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini ambaye pia alikuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amebainisha wanatarajia kumpokea mgombea huyo wa urais na mgombea mwenza wake katika kiwanja cha ndege cha Arusha.
Amesema wagombea hao wanakuja mkoani Arusha kwa ajili ya uthamini wa fomu ya ugombea Urais ,ambapo amewataka wanachama wote wa CHADEMA kujitokeza kwa wingi ,pamoja na viongozi wote wa kanda kujitokeza kumpokea.
‘’Baada ya kumpokea tutakuja naye na wananchama pamoja na viongozi wa Chama waliojitokeza kumleta mpaka ofisini na kufanya mkutan mfupi kwa ajili ya kumdhamini na hutuba fupi itakuwepo hapo na mgombea wetu ataondoka na kuelekea katika maeneo mengine na tayari ratiba zimeshatolewa na maelekezo ya kiofisi.
"Wanachama wetu wajiandae tu kwa ugeni huo,niwatake tu wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kumthamini mgombea na safari hii sisi kama chadema tumejipanga kupeleka zaidi ya idadi ya wadhamini ambao Tume wamependekeza,"amesema Lema
Wakati huo huo mchakato kuchukua fomu ya kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa chama hicho kwa upande wa Kanda ya Kaskazini umeaanza leo na wanachama wameshaanza kuchukuwa fomu ila yeye hatachukuwa fomu wiki hii.
Bali atatangaza rasmi siku ambayo atachukuwa fomu ,na yeye ndie mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini na hatagemei Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)waseme kuna mgombea mwngine wa Chadema atakayesimama jimbo la Arusha Mini .
“Tunaendelea kuangalia jinsi uchukuaji wa fomu unavyoenda na tuna watu kila upande wanafatilia suala hili kila mahali na niseme hatutakubali matendo maovu yaliyofanywa kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa ujirudie kipindi hiki,"amesema.
Ametoa mwito kwa Jeshi la Polisi kuendelea kutiii sheria bila shuruti ,kama vile wanavyowaelekeza wananchi kutii sheria bila shuruti huku akiwataka wandelee kuwa wapole kama vile walivyoanza mwanzo.
Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya kaskazini ambaye pia alikuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza leo katika ofisi za kanda za chama hicho mblele ya Waandishi wa habari ambapo alibainisha kuwa wanatarajia kumpokea mgombea huyo wa urais pamoja na mgombea mwenza wake katika kiwanja cha ndege cha Arusha ambapo alisema watakutana katika mzunguko wa kisongo (picha na Woinde Shizza,Arusha )
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...