Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akielezea jambo wakati wa kikao chake na Makamishna wa Uhifadhi nchini, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha (aliyevaa uniform za JWTZ , kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi – Usimamizi wa Sheria na Mikakati ya Ulinzi na Usalama, John Nyamhanga ( kulia) wakifurahia jambo kufuatia michango ya wajumbe wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Washiriki wa Mkutano wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kupitia na kuhuisha Miundo ya Taasisi ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi. Mkutano huo ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi, umefanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Kutoka kulia ni Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, William Mwakilema na Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Emmanuel Wilfred. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuzipitia vema sheria za Uhifadhi ili kuwezesha utekelezaji wenye ufanisi utakaoleta matokeo chanya na ya haraka katika Jeshi la Uhifadhi huku Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akifuatilia vema maelezo ya Naibu Katibu Mkuu Dr. Allan Kijazi.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini mkubwa, kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Rasilimaliwatu Witness Shoo ( aliyesimama ) akijibu swali lililohitaji ufafanuzi kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha ( aliyevaa uniform za JWTZ wa tatu kutoka kushoto kwa Witness Shoo. 

***************************
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akiongoza kikao cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi ( organization structures ) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za Uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...