Na,Jusline Marco-Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Kenani Kiongosi amewataka wananchi kulinda na kutunza miundombinu ya reli ili kuweza kuendelea kunufaika na huduma za treni katika jiji la Arusha na maeneo ya jirani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Kimanta katika hafla fupi ya kupokea treni ya kwanza ya mizigo ya majaribio,Kenani amesema kuwa ni jikumu la kila mmoja kutunza na kulinda miundombinu hiyo.
Aidha amesema kuwa ujio wa treni hiyo ni fursa kwa kila mwananchi na mkazi wa jiji la Arusha hususani wafanyabiashara na wajasiriamali katika kuendeleza biashara zao.
Aidha ameeleza kuwa ukarabati wa reli hiyo umegharimu zaidi ya bilioni 14 huvyo ujio wa treni hizo utawanufaisha wafanyabiashara kutokana na mizigo yao kusafirishwa kwa wakati na kwa gharama ndogo na kufungua fursa ya kiuchuki katika mkoa na wilaya ya Arusha.
"Wananchi mnajukumu la kuhakikisha mnalinda watu wasije wakaharibu miundombinu ya reli,kwasababu miundombinu ikihujumiwa treni haitafika hapa na treni isipofika hizi faida zote hazitaoweza kuonekana."Alisisitiza Kenani
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amesema kuwa ujoo wa treni hiyo imetokana na kukamilika kwa ukarabati wa reli ambayo ilisimama kwa muda wa miaka 30 kuendesha shughuli za usafishaji katika mkoa huo ambapo juo huo unaashiria kukamilika kwa mchakato ya kuanza kupokea treni ya pili abiria mwishoni mwa mwezi huu.
"Huu ni udhihirisho wa kazi kubwa inayofanywa kwa kipindi cha miaka 5 ya muheshimiwa rais Dkt.John Magufuli na niendelee kumshukuru Mhe.rais kwa kuendelea kutuamini sisi vijana na tunaendelea kuchapa kazi "Alisema Mkuu huyo wa wilaya
Naye Kiongozi wa kituo cha treni Atusha mjini Victor Nicolaus amesema kuwa ujio wa treni hiyo unafungua rasmi shirika la reli kuanza huduma zao katika mkoa wa Arusha kwani wananchi wa mkoa huo kwa muda mrefu wamekuwa na matatizo ya usafiri kwa njia ya treni ambayo kwa sasa yametatuliwa.
Ameongeza kuwa wanategemea kuwa wanasafirisha mizigo na abiria kwenda sehemu yoyote ikiwemo mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Dar es salaam ambapo kufufuka kwa njia hiyo kunaleta matumaini mapya kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani waliojitokeza kuipokea treni ya kwanza ya majaribio ya mizigo leo ikitokea jijini Dar es salaam hadi Mkoani Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Kenani Kiongosi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakiwasili na reli ya kwanza ya majaribio ya mizigo iliyowasili leo jijini Arusha baada ya kipita miaka 30 bila kuwepo kwa huduma za usafiri kwa njia ya treni.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...