Na
Mwandishi wetu, Tabora.
BENKI
ya Mwalimu (Mwalimu Commercial Bank Plc) imewahimiza wanahisa wake wakubwa na
wadogo na wananchi kwa ujumla kutumia huduma za benki hiyo kwani inazidi
kuimarisha miundo mbinu yake ili kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi nchi nzima.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Mkutano mkuu wa nne wa wanahisa wa benki hiyo katika ukumbi
wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora Agosti 13, 2020, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO)
wa Benki hiyo Bw. Richard Makungwa alisema benki itaendelea kuimarisha miundo
mbinu yake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara ambapo hadi hivi sasa licha
ya kuwa na matawi mawili ya Dar es Salaam, Benki ipo mbioni kufungua tawi la
tatu jijini Dodoma kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2020.
“Tuna
huduma za Mwalimu Mobile kupitia *150*31#, vile vile huduma ya Mwalimu Wakala
(mpaka sasa tuna mawakala wapatao 90 wanaopatikana nchi nzima). Wateja wetu
wanaweza pata huduma za ATM kupitia UMOJA Switch na wanaweza kuweka hela
kupitia matawi yote ya TPB Bank nchi nzima. Vilevile tunatarajia kuanza kutoa
VISA Card kwa wateja wetu kabla ya kufikia mwishoni mwa mwaka huu.” Richard
Makungwa, Afisa Mtendaki Mkuu Mwalimu Commercial Bank.
Alisema
Benki itaweka mazingira mazuri ya biashara ili walimu binafsi wanahisa kwa
ujumla kutumia huduma za Benki hiyo katika kukata bima za mali na maisha yao
kupitia Benki ya Mwalimu ambayo sasa ni wakala wa bima.
Alisema
kwa kufanya hivyo Wanahisa wote kwa ujumla wahamasike kutumia huduma za benki
hiyo katika kufanyia shughuli zao zote za kifedha kuiwezesha Benki kujiongezea
mapato ili kuharakisha muda wa kutoa gawio kwa wanahisa.
“Benki
pia inategemea mapato kutoka katika miamala mbalimbali kama kutoa pesa kwenye
akaunti, kutuma fedha kupitia simu vile vile kutuma pesa kwa mfumo wa kibenki
(mf. TISS/EFT) na huduma za kibenki kupitia mawakala wetu.” Alisisitiz Afisa
Mkuu Mtendaji.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Deus Seif. Alisema…“Walimu
naomba tutumie benki yetu…tutumie benki yetu, kuna sehemu tulizembea kidogo,
wakati viongozi wetu wa Chama Cha Walimu wanaanzisha hii benki waliamini kwamba
benki itakuwa na nguvu kuliko mabenki yote kwasababu waliamini walimu wasiopungua
217,000 walioko kwenye pay roll ya Januari 2015 wote watafungua akaunti na
kuitumia benki yao na inamaan sasahivi ingekuwa benki kubwa na yenye nguvu,
pamoja na changamoto zote hizi lakini tujitahidi kutumia benki yetu.”
Akisisitiza
kuhusu umuhimu wa ushiriki wa dhati wa walimu katika benki hiyo Rais wa CWT,
Mwl. Leah Ulaya alifafanua kuwa “Mimi kama kiongozi wa walimu hapa Tanzania
nitumie nafasi hii kwanza kuwapongeza kwa maamuzi tuliyofikia leo lakini pia
niendelee kuwasihi na kuwaomba wanahisa wenzangu ambao ni walimu tuendelee
kuona umuhimu wa kuendelea kuithamini benki yetu na kadiri bodi yetu
itakavyotuelekeza wakati utakapofika tupeleke mishahara yetu kwenye benki ya
Mwalimu tusisite kufanya hivyo
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bw. Herman Mark Kessy alisema
Mkutano huo wa wanahisa ni muhimu sana kwa sababu pamoja na kupata taarifa
rasmi kuhusu mwenendo na utendaji wa Benki, pia umetoa nafasi ya kujadili mambo
mbalimbali na kuyafanyia maamuzi.
“Nichukue
fursa hii kuwashukuru sana tena sana kwa kuniamini, mimi ninaamini hii benki
inakwenda kufanya vizuri sana, kama mkiangalia katika benki zilizoko hapa
nchini Mwalimu Commercial benki ndiyo benki ya wazalendo halisi….benki hii
ndiyo yenye wanahisa wengi zaidi kuliko benki nyingine yeyote ile ina wanahisa 217,000
katika benki zote zilizo kwenye orodha ya soko la hisa la Dar es Salaam.” Herman
Kessy, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...