Na Woinde Shizza 

Wito umetolewa kwa wanachama na wafuasi wachama Cha mapinduzi kuacha unafiki badala yake kusimamia ukweli na kukitafutia kura Chama hicho ili kiweze kushinda kwa kishindo . 

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Wilaya ya kichama ya Arumeru Saimon Saning’o wakati akiongea katika mkutano wa kampeni za kumuombea kura mbunge wa wa Jimbo la Arumeru Magharibi Noah Lembris ,Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli pamoja na diwani wa kata ya Tarakwa mkutano uliofanyika katika viwanja vya miti Mitimitatu. 

Alisema kuwa ni wajibu wa kila mwanachama Kuhakikisha anakiangaikia chama Cha mapinduzi kipite kwa kishindo na sio kuanza kukaa nakuanza kuwafitinisha wagombea ambao wamepitishwa na chama hicho. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato Alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi waliokuwa na uchu wa madaraka ambao waligombea nafasi mbalimbali lakini baada ya majina Yao kukatwa wamekisaliti chama na wameenda upande wa pili Jambo ambalo Sio zuri na hawatalifumbia macho. 

“uchaguzi uliopita mlifanya kosa mkampa mtu anaejali maslai yake badala ya kujasali maslai ya ya wananchi na ndio maana tangu mumpe uongozi ameshindwa hata kuwatengenezea barabara ,nijambo la haibu mtu kapewa ridhaa na wananchi miaka mitano yote hamna ata shule ya msingi katika kata hii sasa niwaambie kipindi hichi msifanye kosa tena bali chagueni kiongozi ambaye atawaletea maendeleo ambaye anatokea CCM”alibainisha Omary 

Akiongea na wananchi hao mgombea ubunge wa jimbo hilo Noha Lemburis Mollel alisema kuwa anajua katika kata hiyo kuna matatizo mengi ikiwemo ya ukosefu wa maji ,Barabara ,kituo cha afya na hata shule ya msingi hivyo iwapo watampa ridhaa atahakikisha anatatua changamoto zote hizo . 

“nijambo la ajabu hadi leo hii amna shule ya msingi ya Tarakwa ,hamna kituo cha afya cha kata hii nisema tu mkinipa ridhaa mambo ambayo nitaanza nayo ni haya mawili lakini pia nitahakikisha barabara zinajengwa na maji yanakuja na uzuri zaidi serikali ya awamu ya tano ilileta mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520 na katika mradi huo Rais aliagiza vijiji vyote vya jirani vilivyopitiwa na mradi huo vipewe maji sasa na mimi niwakikishie tu kijiji hichi nacho nitahakikisha kinapatiwa maji “alisema Noah 

Aidha kwa upande wa ajira aliwataka vijana kutochagua kazi bali wafanye kazi yeyote ambayo ambayo itawaingizia kipato mradi isiwe ya wizi ,na kuwataka wachape kazi usiku na mchana ili waondokane na umaskini ,huku akiwasihi wasiogope kwenda kuchukuwa mikopo iliotengwa na serikali kwa ajili ya vijana ili wafungue biashara zao na waweze kuendesha maisha yao. 

kwa upande wake aliekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia walemavu Amina Mollel aliwataka wananchi hao wasifanye makosa tena ,bali wamchague magufului kwani ni kiongozi ambaye anajali watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama na ndio maana ameweza kuwaletea miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo .
aliekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia walemavu Amina Mollel akiwa amelala Chini akimuombea Rais ,mbunge na diwani kura katika mkutano uliofanyika kata ya Tarakwa uliopo Wilayani Arumeru
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato Akiongea na wananchi katika mkutano huo 
Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Wilaya ya kichama ya Arumeru Saimon Saning’o Akiongea na wananchi wa kata ya Tarakwa 

**************************************

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...