Na Woinde Shizza, Vero Ignatius Michuzi TV Arusha
Zikiwa zimesalia siku 29 nchi ya Tanzania iingie kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 wa kumchagua Rais,wabunge na madiwani,wananchi wametakiwa kuilinda Amani,utulivu pamoja na kufuata taratibu na kanuni za nchi
Mkurugenzi Mkuu wa uchaguzi Dkt.Charles Mahera akizungumza na wadau wa Taasisi za kiraia,Viongozi wa dini ,wazee wa Kimila lna watu wenye mahitaji maalum alisema Tume imejipanga kuwa na Uchaguzi wenye utulivu wa hali ya juu.
Dkt Mahera alisema kuwa Kati ya wapiga kura 29,188,347 walioandikishwa wanawake ni 14,496,604 ambao ni sawa na 49.67%,vijana wenye umri wa Miaka 18-35 ni 15,650,998 Vijana wa kiume Ni 7,804,845 na wa kike Ni 7,846,153
Aidha kuna jumla ya watu wenye ulemavu 13,211na Kati yao 2,223 Wana ulemavu wa macho ,4,911 Wana ulemavu wa mikono,6,077 Wana ulemavu wa aina nyingine
Alibainisha kuwa tume hiyo itatumia vituo vya kupigia kura 80,155 katika zoezi la kupiga kura tarehe 28/9/2020 ,Kati ya vituo hivyo Tanzania Bara itakuwa na vituo 79,670 na Tanzania Zanzibar itakuwa na vituo 685 pia itatumia vituo 1,412 vya NEC kwa upande wa Zanzibar tume imeridhia mipaka ya majimbo Kama ilivyorekebishwa na tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kila kituo Kati ya hivyo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500
Aidha aliwataka wadau hao kwenda kutoa Elimu kwa jamii na kuwaasa kwenda kumsikiliza Sera ili waweze kumchagua kiongozi wanaompenda
Akichangia Mara katika kikao Askofu wa Kanisa la Menonite Amos Mhagachi alisema kuwa Ni vyema take makundi yanayifanya fujo katika kipindi Cha Kampeni wachukuliwe hatua za kisheria ili Amani iliyopo uendelee kutunzwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...