Zaidi ya Bilioni 3 zinakusanywa kila mwaka  katika Pori la Akiba la Lukwati/Piti  lililopo Mkonia Songwe chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA), ambapo ni miongoni mwa  mapori ya akiba 23 yanayosimamiwa na mamlaka hiyo. 

Hayo yamesemwa na Meneja wa pori hilo Bw. Jembe Chifuno mbele ya  Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania-TAWA Bw. Mabula Misungwi akiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi katika kukagua mapori yanayosimamiwa na TAWA.

Aidha Bwana Chifuno memueleza kaimu Kamishna Mabula  kuwa pori hilo  lina vivutio vingi vya utalii wakiwepo wanyamapori mbalimbali  ambao ni kivutio kikubwa  cha  wageni wengi kutoka nchi mbalimbali duniani kote kuja kujionea wanyama hao.

Hata hivyo Shughuli za uwindaji ndio sababu kubwa iliyosababisha Pori hili kuwa kinara wa ukusanyaji wa mapato, ambapo mwaka 2018 pori liliingiza Jumla ya Dola za kimarekani 550,000 sawa na Tshs billioni 1.2  na mwaka 2019 ,waliingiza Dola 632,000 sawa na Tshs. billioni 1.4.

Nae Kamishna Mabula Misungwi baada ya kuelezwa hayo alionesha kufurahishwa na kuridhishwa na jitihada zinazofanywa na watumishi wa pori hilo katika kutunza, kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa walizopewa  kuzisimamia  Awari Wakizungumza mbele ya Kaimu Kamishna huyo watumishi wa pori hilo walishauri mambo mbalimbali ikiwemo Kuanzishwa kwa utalii wa picha kwani yapo maeneo mengi rafiki kwa aina hiyo ya Utalii.

Mengine ni kugawanywa kwa Pori  katika Kanda kurahisisha utekelezaji mzuri wa majukumu yao kwani pori lina ukubwa wa Kilometa za mraba 6,113 ambazo ni kubwa Sana kiutendaji,Waliomba waongezewe vitendea kazi kama vile magari ya doria,mahema na doria za anga kwa kutumia ndege za TAWA na  Kuongeza idadi ya watumishi.


Akijibu changamoto za watumishi hao Kaimu Kamishna Mabula aliwapongeza watumishi kwa juhudi kubwa walizofanya kulisafisha pori kwa kuimarisha ulinzi na kuwataka waongeze juhudi na kuahidi kushughulikia changamoto zaidi kadri wawezavyo ili kuongeza morali ya watumishi na mapato.

 

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...