Wahitimu wakiburudika katika mahafali ya 13 yaliyofanyika mwishoni mwa juma(Septemba 26, 2020).
Mkurugenzi Mtendaji wa Mutembei Holding Limited (MHL), Peter Mutembei akizungumza katika Mahafali ya 13 ya shule ya Sekondari Vikitory yaliyo fanyika mwishoni mwa wiki Septemba 26 wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

Na Avila Kakingo, Globu ya jamii
TAASISI ya inayoongoza shule za sekondari na msingi za Mutembei Holding Limited (MHL) inatimiza miaka 23 mwaka huu 2020 tangu ianze kutoa huduma ya elimu hapa nchini.

Shule zinazoongozwa na taasisi hiyo ni shule ya sekondari Ujenzi, Shule ya Sekondari Victory, Shule ya Sekondari na Msingi ya St. Methew's zilizopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Shule ya Sekondari St. Mark's iliyopo jijini Dar Es Salaam na shule ya Image Vosa iliyopo Mkoani Iringa.

Akizungumza wakati wa Mahafali 13 ya shule ya Sekondari Victory yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Septema 26, 2020 Mkurugenzi Mtendaji wa Mutembei Holding Limited (MHL), Peter Mtembei alisema kuwa wanauzoefu wa kutosha katika kutoa huduma ya elimu katika jamii.

"Mwaka huu 2020 taasisi inayongoza shule ya Sekondari Victory inayoongozwa na Thadeo Mutembei inatimiza miaka 23 ya kuhudumu katika elimu. Nathubutu kusema tunauzoefu wa kutosha na tumeyaishi mafanikio pamoja na changamoto katika utoaji huduma katika Sekta ya elimu kwa kipindi chote hicho bila kuyumba."Alisema Mutembei

Alisema kuwa kutimiza miaka 23 sio jambo dogo na elimu inaendela kutolewa huku wakiwa na malengo kadha wa kadha ili  kuhakikisha wanafunzi wanapomaliza shule wanatoka wakiwa wameelimika, wanamaadili mema pamoja na kuwa na ujuzi stahiki unaowawezesha kumudu changamoto za maisha.

Mutembei alisema kuwa ili kuhakikisha wanasimama katika misingi waliyojiwekea wanahakikisha wanasisimama kufanya tathmini na mapitio mara kwa mara ya matokeo na utendaji wao katika utoaji huduma.

Alisema kuwa baada ya kutoridhishwa na utendaji wao kwa mwaka 2018 walilazimika kufanya marekebisho na maboresho mwaka 2019 ili kuleta tija katika utendaji wao. Lengo likiwa ni kuhudumia kwa ukaribu kila mtoto wakiwa na malengo matatu.

Lengo la kwanza ilikuwa ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu iliyo bora, lengo la pili ni kuhakikisha kila mtoto anapatiwa malezi mazuri shuleni na jambo la tatu ni kuhakikisha kila mtoto anakuwa salama awapo ndani na nje ya mazingira ya shule.

"Malengo yetu ni kuifanya shule ya Sekondari Victory na shule zote zinaongozwa na MHL kuwa shule bora Tanzania katika Nyanja zote kwani mpaka sasa tumeboresha mazingira ya kujifunzia kuanzia madarasani mpaka nje ya madarasa, tumeboresha Mambweni ili watoto walale mahali pazuri, tumeboresha Maktaba, Maabara za Masomo ya Sayansi kama wazazi mlivyoona katika maonesho ya masomo kwa vitendo kwa wanafunzi wetu hapa shuleni." Alisema Mutembei

Hata hivyo Mtembei alisema kuwa shule ya Sekondari Victory inakuwa na taalumu nzuri kwa sasa wapo katika ukarabati wa darasa maalumu ambapo wanafunzi watafundishwa kwa njia ya Teknolojia ambapo watoto watajifunza kwa kupitia Mfumo wa Sauti na kuona (Video yaani Audio Visual Class.) Alisema kuwa darasa hilo litasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuongeza uelewa na ufaulu katika shule hiyo.

Hata hivyo Mutembei alisema kuwa Changamoto ya Ugonjwa wa Corona imechelewesha baadhi ya mambo lakini kwa sasa ugonjwa huo umepungu sasa wanampango wa kupeleka watalamu mbalimbali katika nyanja tofauti kama wataalamu wa afya, malezi, Saikolojia na fani zingine kwaajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi ili kuhakikisha wanakabiliana na changamoto mbalimbali za maisha mara baada ya shule.

Licha ya hilo kwa upande wa Imani za dini amesema kuwa kila mwanafunzi anapata fursa ya kushiriki mafundisho ya dini ambayo hutolewa kwa lazima kwa kila mwanafunzi kulingana na imani yake katika shule zote zinazomilikiwa na MHL.

Mutembei aliwaomba wazazi waendelee kuwaamini na kuwaunga mkono na kuwapelekea maoni pale ambapo wanaona panahitaji kuboreshwa na wao uongozi wa shule watachukua hatua katika kuboresha.

Amesema yote hayo yanawezekana kutokana na kuwa na timu nzuri ya walimu na wafanyakazi wasio walimu wao hakikisha kila kitu kinaenda vizuri shuleni hapo. Na amewashukuru sana wafanyakazi wote shuleni hapo kutokana na kazi wanazozifanya za kulea wanafunzi shuleni hapo na kuishi nao vizuri.

Hata hivyo Mutembei ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani wanafunzi wamezidi kuongezeka katika shule hiyo na taaluma wamekuwa wakifanya vizuri kutokana na serikali kuboresha katika sekta ya Elimu.

"Katika kipindi cha janga la Corona serikali imesimama kidete kutuongoza chini ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuvuka salama na kuhakikisha watoto wetu wanarudi shuleni kwani walikuwa hawajui hatima yao ya kumaliza kidato cha nne, lakini serikali yetu imesimamia hilo na kurudi shule na hivi leo wa kidato cha nne wanahitimu." Alisema Mutembei.

Hata hivyo Mutembei aliwapongeza Kidato cha nne. "Hongereni sana vijana waNaamini mtaendelea kuonesha maadili, ujuzi, maarifa, uelewa mtakapo kuwa nyumbani."
Walimu wa shule ya Sekondari Victory wakiwa mbele ya jukwaa katika mahafali ya 13 yaliyofanyika mwishoni mwa juma(Septemba 26, 2020).
Baadhi ya wahitimu.
Meza kuu  wakifurahia jambo katika mahafali ya 13 yaliyofanyika mwishoni mwa juma(Septemba 26, 2020).
Burudani ya Wahitimu ikiendelea.
Changanyikeni wazazi walezi na wanafunzi burudani ikiendelea katika mahafali ya 13 yaliyofanyika mwishoni mwa juma(Septemba 26, 2020).
Wanafunzi wanaobaki wakitumuiza katika mahafali ya 13 yaliyofanyika mwishoni mwa juma(Septemba 26, 2020).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...