Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akieleza suala la Ushirika wakati wa majadiliano ya Uchambuzi utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ushirikiano na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dodoma, Septemba 24, 2020.
Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Sabina Seja akifafanua jambo wakati wa Kikao cha kujadili uchambuzi wa Mfumo wa utendaji wa Vyama vya Ushirika wa Mazao Nchini kutokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa ushirikiano na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, kikao kilichofanyika Jijini Dodoma, Septemba 24, 2020.
Wajumbe wa Kikao kilichokuwa wakijadili Uchambuzi wa Mfumo wa Utendaji wa Vyama vya Ushirika wa Mazao nchini kutokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ushirikiano na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dodoma, Septemba 24, 2020.


========  ========  ==========

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) kwa kushiriana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika zimeazimia kuendeleza jitihada za kuimarisha na kuboresha Sekta ya Ushirika nchini ili kuondokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza katika Sekta ya Ushirika.

Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Sabina Seja akiongea wakati wa kikao cha kujadili uchambuzi wa Mfumo wa Utendaji wa Vyama vya Ushirika kutokana na utafiti iliyofanywa na TAKUKURU kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika amesema Taasisi hiyo imechukua hatua hiyo ya ushirikiano ili kuokoa mali za Ushirika pamoja na kuimarisha Utawala Bora. Kikao kilichofanyika Septemba 24, 2020 katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Jijini Dodoma. 

Akifafanua lengo kuu la Utafiti huo Mkurugenzi huyo alieleza Utafiti huo utasaidia Taasisi hizo kwa pamoja kutathmini utendaji na uendeshaji wa vyama vya Ushirika wa mazao kwa kubainisha maeneo yenye viashiria vya Rushwa ili kupendekeza namna bora ya kuimarisha mfumo wa uendeshaji na Usimamizi wa Vyama hivyo.

Aidha, ilielezwa kuwa baadhi ya maeneo mahususi yaliyozingatiwa katika utafiti huo ni pamoja na kutathmini mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa Ushirika wa mazao, kutathmini ufanisi wa mifumo ya ndani na kubainisha mianya ya rushwa katika utendaji wa Ushirika wa Vyama vya mazao.

Katika kikao hicho Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu Dkt. Benson Ndiege amesema Tume itaendelea kushirikiana na wadau katika kuimarisha na kuhakikisha kuwa Ushirika unaendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Ushirika. Mrajis aliongeza kuwa mfumo wa uendeshaji wa Vyama vya Ushirika unaweza kuimarishwa kwa kuzingatia masuala mbalimbali ikiwemo kuangalia sifa za watendaji wa Vyama, taratibu za uendeshaji wa Mikutano ya Wanachama pamoja na utoaji wa huduma kwa Wanachama. 

“Ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika kuimarisha utawala bora kwenye Vyama vya Ushirika ni vizuri kuendelea kuangalia kwa karibu zaidi namna mifumo ya udhibiti ya ndani inayohusisha mambo mengi kama vile usomaji wa taarifa za fedha, ukaguzi wa vyama,” alisema Mrajis

Pamoja na mambo mengine, baadhi ya Changamoto zilizobainika katika utafiti huo ni pamoja na uelewa mdogo wa masuala ya uendeshaji na usimamizi wa Ushirika kwa watendaji pamoja na wanachama wa Ushirika. Hivyo utafiti huo pamoja na majadiliano ya kikao hicho yalipendekeza kuongeza utoaji wa elimu ya Ushirika kupitia njia mbalimbali ikiwemo matumizi ya Vyombo vya Habari katika kuelimisha Wanachama wa Vyama vya Ushirika Misingi ya Ushirika, Haki na Wajibu wa Mwanachama pamoja na majukumu ya Chama kwa Wanachama wake.

Kikao Kazi hicho kimehudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Ushirika Ikiwemo Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) pamoja na Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...