Na Jusline Marco -Arusha


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Dkt.Charles Mahera amevikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wananchi kujihadhari na vitendo vitakavyopelekea uvunjifu wa amani pamoja na matamshi mabaya katika kipindi hiki cha kampeni.


Ameyasema hayo katika mkutano wake na wadau wa uchaguzi M-koa wa Arusha kuwa tume imejipanga kusimamia uchaguzi kwa kufuata katiba ya nchi ya mwaka 1977, sheria za uchaguzi,kanuni na miongozo mbalimbali.


Aidha Amefafanua kuwa katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura Tume ilitumia billioni 157 na katika zoezi la uchaguzi inatarajia kutumia Bilioni 331 ambapo tayari wamesapokea zaidi ya bilioni 20 na maandalizi yametimia kwa zaidi ya asilimia 80.


Pamoja na hayo Tume iliboresha maelekezo mbalimbali ya uchaguzi kwa ajili ya wadau na watendaji wa uchaguzi ambapo maelekezo hauo yalitolewa kwa wasimamizi wa uchaguzi,vyama vya siasa,wagombea,wasimamizi wa vituo,mawakala wa vyama vya siasa pamoja na makarani waongozaji wapiga kura.


Vilevile Dkt.Mahera ameongeza kuwa Tume itatumia vituo vya kupigia kura vipatavyo 80155 katika zoezi la kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu kati ya vituo hivyo Tanzania Bara ni vituo 79670 na Tanzania visiwani vikiwa 485 ambapo vituo vitakavyotumiwa na Tume vya ZEC kwa upande wa Tanzania visiwani ni vituo 1412 huku kila kituo kati ya hivyo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.


Ameongeza kuwa katika kufanikisha uchaguzi wa mwaka huu,Tume imeendelea na utekelezaji wa shughuli mbalimvali zilizoainishwa kwa mujibu wa sheria na tayari imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili ambapo zoezi la uboreshaji wa daftari kwa awamu zote mbili wapiga kura ambao taarifa zao zimejirudia na wale waliokosa sifa waliondolewa.


Dkt.Mahera ameeleza kuwa hivi sasa daftari lina jumla ya wapiga kura 29188347 ambapi wapiga kura 29059507 wapo Tanzania Bara na wapiga kura 128840 wapo Tanzania visiwani,hali kadhalika kuna jumla ya wapiga kura 566352 walioandikishwa na ZEC ambao watashiriki kupiga kura ya kumchagua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Sambamba na hayo ameongeza kuwa kati ya wapiga kura 29188347 walioandikishwa wanawake ni 14691743 sawa na asilimia 50.33,wanaume 14496604 sawa na asilimia 49.67,Vijana wenye umri kati ya 18 hadi 35 ni 650998 ambapo vijana wakiume wakiwa 7804845 na vijana wa kike ni 7846153,watu wenye ulemavu 13211 kati yao 2223 wana ulemavu wa kuona,4911 wana ulemavu wa mikono na 6077 wakiwa na ulemavu wa aina nyingine.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo la Arusha mjini Dkt.John Pima amevipongeza vyama vyote kwa kuendelea na kampeni za utulivu na amani ambapo amewataka kukemee makundi ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaleta hali ya vurugu.


Kwa upande wao baadhi ya wadau wa uchaguzi katika mkutano huo likiwemo kundi la watu wenye mahitaji maalum wameionga Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweka wakalimani wa lugha za alama katika vituo vya kupigia kura ili kuwawezesha nao kushiriki zoezi hilo kikamilifu.


Hata hivyo uchaguzi  wa Rais, wabunge, na madiwani unatarajiwa kufanyika October 28 mwaka huu ambapo kauli mbiu inayolnguza uchaguzi ni “ Shime mwananchi jitoleze kupita kura siku ya uchaguzi kwani Kura yako ni sauti yako nenda ukapige kura.

 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Charles Mahera akizungumza na wadau wa uchaguzi Mkoa wa Arusha.

Wawakilishi wa makundi maalum wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,katika mkuwano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...