Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo (akiwahudumia chai) akigawa chai kwa wafanyakazi wake. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imehitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na East African Spirits (T) Ltd vinavyomilikiwa na Mwekezaji Mzawa Gaspar Kileo ambaye amekuwa mteja mkubwa wa Benki hiyo kwa takribani miaka 32.

Akizungumza wakati wa kunywa chai hiyo ya pamoja leo Ijumaa Oktoba 16,2020 katika viwanja vya Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd vilivyopo Ibadakuli Mjini Shinyanga,Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja amesema lengo la chai hiyo ni kuwashukuru wateja wao hao wakubwa.

“Benki ya CRDB inasherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo mwaka huu tulipanga kusherehekia kwa muda wiki mbili.Leo tumefika hapa kwa ajili ya kufunga Wiki ya Huduma kwa wateja hapa katika eneo lenu la kazi ili kuwashukuru kwa kuwa wateja wetu wakubwa”,amesema Segeja.

“Viwanda hivi vimechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Benki ya CRDB ndiyo maana nasi tumeona umuhimu wa kufika hapa ili kusherehekea nanyi wiki ya huduma kwa wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa viwanda hivi”,ameeleza Segeja.

Segeja amewaomba wafanyakazi wa Kampuni hizo kuendeleza  mahusiano na ushirikiano wao kwa Benki ya CRDB huku akibainisha kuwa Benki hiyo inaendelea kupokea maoni ya wateja ili kuboresha huduma za kibenki.

Kwa upande wake, Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice ameishukuru Benki ya CRDB kuandaa chai ya pamoja na wafanyakazi wake.

Kileo maarufu kwa jina la Gaki  ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) ameahidi kuendelea kushirikiana na Benki ya CRDB ambayo wamekuwa wakiitumia kupitishia mishahara ya wafanyakazi wake kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Wakati wa kunywa chai hiyo, Gaki akiwa amevaa Aproni aliongoza zoezi la kuhudumia/kugawa chai kwa wafanyakazi wake ambayo iliandaliwa na benki ya CRDB akisaidiana na viongozi wa Benki ya CRDB akiwemo Beatus Segeja kutoka CRDB Makao makuu, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui, Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney na Meneja Biashara Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo (wa pili kulia) akiwa na Viongozi wa Benki ya CRDB katika viwanja vya Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd) kabla ya kuanza kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akiyashukuru Makampuni ya GAKI kwa kuendelea wateja wa Benki ya CRDB
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akimkabidhi zawadi Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice. 
 Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice akionesha zawadi aliyopewa na Benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akizungumza kabla ya kuanza kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo akiwa amevaa Aproni na viongozi wa Benki ya CRDB na Makampuni ya Gaki akitoa utaratibu wa kuhudumia/kugawa chai kwa wafanyakazi wake kuwa yeye ndiyo ataongoza zoezi kwa kuwahudumia wafanyakazi wake.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo viongozi wa Benki ya CRDB na Makampuni ya Gaki wakiwa wameshikilia vitafunwa wakati wa zoezi la kunywa chai ya pamoja
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo (akiwahudumia chai) akigawa chai kwa wafanyakazi wake. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo na Mkurugenzi Msaidizi wa Makampuni hayo , Humphrey Kileo  ( wa kwanza kushoto) wakigawa chai kwa wafanyakazi wao. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja wakiendelea kugawa vitafunwa/chai kwa wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akigawa chai kwa Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja, kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akigawa chai kwa Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akiwahudumia chai wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI wakiendelea kunywa chai iliyoandaliwa na Benki ya CRDB
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja (katikati), Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney wakinywa chai baada ya kumaliza kuwahudumia wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki.
Wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki wakichukua Juisi
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo akiishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa chai kwa ajili ya wafanyakazi wa makampuni yake.
Wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI wakiendelea kunywa chai iliyoandaliwa na Benki ya CRDB akitoa neno la shukrani kwa uongozi na wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki baada ya kunywa chai ya pamoja.
Viongozi wa Benki ya CRDB wakipiga picha pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd baada ya kumaliza kunywa chai
Viongozi wa Benki ya CRDB wakipiga picha pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Gaki Transport Ltd baada ya kumaliza kunywa chai
Viongozi wa Benki ya CRDB wakipiga picha pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd baada ya kumaliza kunywa chai

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...