
Na Salome Shayo, PSJ
MSANII wa bongo fleva Juma Mussa alimaarufu Jux amethibitisha kuwa miongoni mwa wadada waliocheza kwenye nyimbo yake mpya ijulikanao kwa jina la Siyo mbaya amefanana na Ex girlfriend wake Vanessa Mdee (vee money).
Ameyasema hayo Septemba 30,2020 katika mahojiano ya kipindi cha XXL Clouds FM baada ya kuulizwa swali na mmoja kati ya watangazaji kipindi hicho ambacho hutangazawa na Mamy beby, Kenedy the Remed na Adam Mchomvu. Amesema kuwa nyimbo hiyo inahusu historia ya maisha yake.
“Unajua nyimbo ya siyombaya kama ulikuwa unafatilia uko nyuma nilikuwa nasema kwamba nyimbo ni ya ukweli wa maisha yangu na ya maisha ya watu wengine……………….”
Amehitimisha kusema kwa sasa anafuraha kwasababu hayupo kwenye mauhusiano hivyo inamsaidia kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...