JINA la “Rais wa Tanga” analoitwa mfanyabiashara maarufu jijini Tanga, Yanga Omary Yanga,  limezua mjadala mahakamani alipokuwa akitoa  utetezi wake dhidi ya kesi  inayomkabili ya kusafirisha dawa za kulevya aina na heroin zenye uzito wa gramu 1052.63.

Akijibu maswali ya wakili wa Serikali Constantine Kakula mbele ya Jaji Imakulata Banzi wa mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kanda ya Tanga, kuwa kwa nini amekuwa akifahamika kwa jina la Rais wa Tanga,  Yanga amedai wamekuwa wakimuita Rais wa Tanga kutokana na ukarimu wake, lakini sio kwa sababu ya kujihusisha au kusambaza dawa za kulevya kama inavyodaiwa na upande wa mashtaka.

Hata hivyo hakukubaliana na upande wa mashtaka kuwa, wanamuita Rais wa Tanga kwa kuwa ni msambazaji wa dawa za kulevya na kudai kuwa, hajawahi kufanya biashara hiyo na wala hatakuja kuifanya.

Amedai hayo wakati akijibu maswali ya upande wa mashtaka baada ya kumaliza kutoa utetezi wake mahakamani hapo.

Mbali na Yanga, washtakiwa wengine ni mkewe Rahma Juma na msichana wa kazi Halima Mohamed. 

Mapema akiongozwa na wakili wake Majura Magafu kutoa utetezi, Yanga ameidai mahakama hapo kuwa anafanya biashara halali ya kuuza bidhaa mbali mbali kwa bei ya jumla ambayo humuingizia karibu sh. Milioni moja kwa siku kama faida na kwamba amekuwa akifanya biashara hiyo tangia mwaka 1986.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, alipomtaka kuonyesha nyaraka zozote za biashara hiyo mshtakiwa Yanga hakuweza kutoa nyaraka zozote kuonyesha kwamba alikuwa na biashara mbalimbali, zikiwemo nyaraka zile zinazohusiana na mkopo wa milioni 800m/- alizopata kutoka Benki ya CRDB kuendeshea biashara husika akidai kuwa nyaraka hizo zilichukuliwa na maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya (DCEA) walipoenda kupekua nyumba yake mwaka 2018.

Aidha alipohojiwa na wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla, Yanga iamekiri kuwa na mali kadhaa, nyumba, zaidi ya viwanja 15 na magari, vitu ambayo vinashukiwa na upande wa mashtaka vilipatikana kwa njia ambayo siyo halali.

Hata hivyo,  Yanga amedai kuwa miongoni mwa viwanja hivyo yalikuwa ni mashamba na mapori yaliyokuwa yakimilikiwa na babu zao, ambayo baadaye yalipimwa na kugawanywa kwa wanafamilia, pamoja na yeye.

Mshtakiwa Yanga, na wenzake, wanadaiwa, Oktoba 1, 2018 huko atika eneo la Bombo Jijini Tanga walisafirisha gramu 1052.63 za dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...