Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa akizungumza na watendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) alipotembelea Baraza hilo pamoja na Naibu waziri wake Mhe. Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Hassan Abbasi ambapo ameliagiza Baraza hilo kuanzisha midahalo na mashindano ya  unadishi wa insha za Kiswahili kwa wananfunzi wa shule za msingi na sekondari ili taifa lipate wabobezi wa lugha hiyo. Ziara hiyo imefanyika Desemba 15, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega akizungumza na watendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao hawapo katika picha hii alipotembelea Baraza hilo pamoja na waziri wake Mhe.Innocent Bashungwa( hayupo pichan) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) ambapo ameliagiza Baraza hilo kuwa na namna  bora ya  kubidhaisha lugha ya Kiswahili nje ya nchi.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa akiwa katika picha ya pamoja Naibu wake Mhe. Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi pamoja na watendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) alipotembelea Baraza Desemba 15, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema kuwa lugha ya Kiswahili ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo ni lazima kuikuza na kuiendeleza ili ipate fursa nyingi katika soko la ndani na la kimataifa.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo Desemba 15, Jijini Dar es Salaam alipokua katika ziara ya kutembelea Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) akiwa pamoja na Naibu wake, Abdallah Ulega pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi  ambapo amesema kwamba, watanzania wana wajibu wa kuipenda lugha ya Kiswahili na kuitangaza huku akisistiza kuwa ni jukumu la watanzania kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha.

“Naigiza BAKITA kuanzisha midahalo na mashindano ya uandishi wa insha za Kiswahili kuanzia shule za msingi na sekondari, lengo ni kuwafanya watoto wajue lugha hiyo kwa ufanisi na hatimaye taifa liwe na wabobezi katika lugha hiyo”,alisema Mhe. Bashungwa.

Bashungwa ameongeza kuwa Serikali itahakikisha nyaraka zote za kimahakama zinandikwa na kutafsiriwa katika lugha ya Kiswahili lengo ni kurahisiha mawasiliano ya watanzania katika kuzisoma na kuzielewa   nyaraka hizo, huku akisisitiza kuwa mpango wa Serikali ni kukiongezea Kiswahili thamani katika ukanda wa Afrika na duniani.

Aidha, Bashungwa amesema kuwa Serikali itahakikisha sifa mojawapo ya wageni kufanya kazi nchini ni kujua lugha ya Kiswahili, lengo ni kukiuza Kiswahili pamoja na kukipa heshima kama utambulisho wa nchi.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ulega amesema kuwa, Kiswahili ni bidhaa adhimu ambayo watanzania wanapaswa kujivunia nayo, huku akiwataka wabobezi wa lugha hiyo kutumia fursa zilizopo katika Ukanda wa nchi za Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki kufundisha lugha hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa, vifaa vya kisasa kwa ajili ya kujifunza ukalimani wa lugha vipo katika hatua ya mwisho ya manunuzi ambavyo   upatikanaji wake utasaidia urahisi wa kujifunza ukalimani.

Vilevile, Kaimu Mtendaji Mkuu wa BAKITA Bi. Consolatha Mushi ameeleza kuwa Baraza hilo limepokea maombi kutoka nchi mbalimbali ambazo zimeonyesha nia ya kujifunza Kiswahili, ambapo pia limeandaa machapisho ambayo yatasambazwa katika nchi za Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...