Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Kosmas Nshenye kulia, akimpa  jiko la gesi na godoro Mwalimu wa ajira mpya  Mark Joseph aliyepangiwa kwenda kufanya kazi katika shule ya msingi Mkako  ambapo Halmashauri hiyo imetoa magodoro na majiko kwa walimu wapya 105 waliopangiwa kufundisha katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kukabiliana na gharama ya  maisha na kuwatiamoyo katika majukumu yao ya utumishi wa umma.

Picha na Muhidin Amri

************************************

Na Muhidin Amri,
Mbinga

HALMASHAURI ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma imepokea jumla ya walimu 105 wa ajira mpya kwa ajili ya shule za msingi na sekondari ambao wamepelekwa katika shule mbalimbali ili kupunguza tatizo la upungufu mkubwa wa walimu uliopo  katika halmashauri hiyo.

Kwa sasa Halmashauri hiyo ina upungufu wa walimu 1,102 kati ya mahitaji ya walimu 1,911 kwa shule za msingi waliopo ni 809,  shule za sekondari mahitaji ni walimu 700 lakini  waliopo ni walimu 440 na kufanya kuwa na upungufu wa walimu 260,ambapo kati yao walimu waliofika wa shule za msingi 66 na sekondari 45.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Juma Mnwele, wakati  kutoa vifaa magodoro na majiko ya gesi kwa walimu wapya 105  na fedha taslimu kwa  walimu  tisa wanaofanya kazi katika maeneo  yenye changamoto.

Alisema, licha ya changamoto  ya upungufu wa walimu, hata hivyo amewashukuru kwa dhati walimu wa shule za msingi na sekondari,waratibu elimu kata,maafisa elimu pamoja na wadau  kwa namna wanavyopambana,kujitoa na kujituma kwa ari na mali katika kuwasimamia na kuwapa ujuzi wanafunzi.

Alisema, kutokana na  upungufu huo serikali ndiyo maana serikali  imendelea kuajiri walimu wapya mwaka hadi mwaka, na kuishukuru serikali kwa kuwapatia walimu hao, jambo alilosema halijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo.

Mnwele alisema, walimu hao wapya wanakwenda kuziba upungufu ambapo wote wamewapangia kwenye vituo ambavyo vimeonekana kuwa na uhitaji mkubwa na kwa kutambua jinsi walimu hao wanavyotakiwa kutuliza akili na kufundisha vijana n ahata kwa kuzingatia muda waliokaa  nyumbani wakisubiri ajira.

Alisema, uamuzi wa kuwapa magodoro,majiko pamoja na fedha baadhi ya walimu  ni Utekelezaji wa kuunga mkono jitihada za Rais wetu  Dkt John Magufuri kwa kuwapatia kwa kumpatia kila Mwalimu godoro,jiko dogo lenye mtungi wa gesi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 27.300,000

Hatua ya kuwapa magodoro na majiko ya gesi ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo kuwafundisha wanafunzi kikamilifu na kuwapunguzia mzigo wa gharama ya maisha hasa ikizingatia walimu hao ndiyo mara ya kwanza kufanya kazi za utumishi na hivyo vifaa hivyo vitakwenda kuchochea morali ya kazi kwao.

Alisema,hatua hiyo ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025 inayolenga kuboresha  elimu kwa ngazi zote kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema, halmashauri  inaandaa utaratibu wa kuwapatia kila mwalimu  aliyepata ajira mpya stahiki yake ya fedha za kujikimu kwa siku saba.

Alieleza kuwa,halmashauri katika mpango wake wa shughuli za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imepitisha mpango wa kutoa motisha kwa walimu wanaofundisha na kuishi kwenye maeneo yenye changamoto ambapo imetoa shilingi 4,500,000 kwa walimu tisa ambao kila mmoja amepewa shilingi  500,000.

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Kosmas Nshenye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo,amewataka walimu hao  kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuleta ufanisi badala ya kuwa sehemu ya malalamiko.

Amewapongeza walimu hao kwa kupata ajira,  hasa ikizingatia kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya walioomba nafasi ya kazi, lakini wao ndiyo waliobahatika kupata nafasi katika halmashauri hiyo.

Amewataka kwenda kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kutumia maarifa sambamba na kuwapenda wanafunzi watakaowakuta shuleni ili kuinua kiwango cha elimu.

Aidha,amewataka kutunza vifaa walivyopewa ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuwaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wana simamia matumizi ya vifaa hivyo kwani vifaa hivyo ni vya serikali na vimenunuliwa kwa ajili ya walimu na sio watu binafsi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Desdelius Haule alisema, jambo  lililofanywa  la kutoa vifaa lililofanywa na halmashauri hiyo  ni historia, kwani hakuna halmashauri za wilaya hapa nchini  ambazo zimetoa vifaa kama hivyo kwa walimu na kumpongeza mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri kwa kubuni mpango huo ambao unakwenda kuinua kiwango cha elimu kwa wilaya ya Mbinga.

Amewataka walimu hao kwenda kufanya kazi na kujiepusha kufanya mambo kinyume na maadili ya utumishi wa umma na kuhakikisha wanakwenda kuwa mfano mzuri, badala ya kuwa watu wa ovyo katika jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...