Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Kufuatia kusimama kwa ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA)  kilichopo katika kata ya Lugarawa kijiji cha shaurimoyo wilayani Ludewa kwa takribani miaka mitatu hatimae ujenzi huo kuanza tena Januari 2021 baada ya upatikanaji wa fedha za kuendeleza ujenzi huo kufikia hatua za mwisho.

Akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi huo meneja mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA Injinia Benitho Mgava kutoka VETA kanda ya Iringa mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema kuwa awali ujenzi ulipangwa kukamilika kwa miezi nane na  kugharimu Bilioni 9 mpaka kuisha ujenzi huo.

Alisema zoezi hilo lilishindwa kukamilika kwakuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi hiyo alitumia fedha hizo kusawazisha eneo la ujenzi badala ya kujenga.

Aliongeza kuwa kwa juhudi za uongozi wa VETA walijaribu kuona namna ya kupata pesa ya kuendeleza ujenzi huo ambapo ilifanikiwa kutenga bilioni 2 ili kusogeza ujenzi lakini kabla fedha hizo hazijatumika wizara ya elimu ikamteua Arusha Technical College kuwa mshauri na kusimamia miradi yote iliyokuwa chini ya ADB.

" Mpaka Sasa eneo hili tayari limeshafanyiwa michoro na kukabidhiwa kwa katibu wa wizara ya Elimu ambapo wameridhia na kukubali kutoa fedha kwa njia ya force account badala ya kupitia kwa mkandarasi na mpaka kuisha kwake utagharimu bilioni 6 ", Alisema Mgava.

Aidha kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya amemtaka kutoa ahadi hiyo ya muda wa  kuanza ujenzi kwa maandishi kwani kumekuwa na maelezo mengi ambayo hakuna utekelezaji wake.

Amesema wananchi walitoa maeneo hayo wakitumaini chuo kitajengwa Kama ilivyopangwa lakini wanavyoona utekelezaji hakuna imefikia hatua wanadai maeneo yao ambayo waliyatoa kwa ujenzi wa chuo hicho ili waendelee na shughuli zao.

" Wananchi waliyatoa maeneo Haya kwa moyo wote wakitumaini watoto wao watapata elimu ya ufundi hapa sasa mnapochelewesha mnapelekea kupoteza imani kutoka kwa wananchi hawa", Alisema. Rubirya.

Naye Mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga alisema chuo hicho kikikamilika kitakuwa msaada mkubwa kwa vijana kwani watapata ajira katika ujenzi na kwa wale watakaosoma ufundi watakuwa watendaji wazuri Pindi utakapoanza mradi wa Liganga na Mchuchuma.

"Wazawa wanatakiwa kuwa vipaumbele katika kupata ajira katika miradi iliyo ndani ya wilaya sasa watapataje ajira hizi wasipokuwa na ujuzi? Kwahiyo chuo hiki kikiwajengea vijana wetu ujuzi itasaidia vijana kupata ajira katika rassilimali zilizo katika wilaya yao", Alisema Kamonga.

Amesema atakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwakuwa ana historia kubwa na eneo hilo kwani yeye ndiye aliyetoa hati ya eneo hilo wakati alipokuwa afisa ardhi wa wilaya hiyo.

Eneo la chuo Cha Veta lililosimama ujenzi wake kwa takribani miaka mitatu.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akielezea umuhimu wa chuo Cha VETA kwa wananchi wake.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kusikiliza hatma ya mradi wa ujenzi wa chuo Cha VETA baada ya  mkuu wa mkoa kuwasili katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya akiongea na meneja wa mradi wa chuo Cha VETA hayupo pichani pamoja na wananchi.

 Meneja mradi wa ujenzi wa chuo Cha VETA kutoka Kanda ya Iringa Injinia Benitho Mgava akitoa maelezo juu ya mradi kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya pamoja na mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga(Hayupo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...