KIKOSI cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC tayari kimewasili jijini Dodoma kikitokea Mbarali Mkoani Mbeya kuwakabili Mafande wa JKT Tanzania mchezo utakaopigwa Disemba 23 katika uwanja wa Jamuhuri Jijini hapa.

KMC FC ambao ni wageni katika mchezo huo watakuwepo Jijini hapa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na hivyo kuhakikisha kwamba wanaodoka na alama tatu dhidi ya JKT Tanzania.

Licha ya kwamba KMC FC imepoteza michezo mitatu mfululizo, Makocha John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo wanaendelea kukisuka kikosi hicho cha wana Kino Boys ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha kwamba wanaondoka na alama tatu wakiwa Makao Makuu ya Nchi.

“Hali ya kikosi kwa ujumla iko vizuri, pamoja na kwamba tulipoteza mchezo wetu dhidi ya Ihefu lakini bado tunamatumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu unaofuatia, zaidi pia tunayafanyia kazi makosa ambayo yalifanyika katika mchezo wetu uliopita.

Kikubwa ni kwamba hatuzarau Timu, hakuna timu nyepesi katika mchezo, ndio mana tumekuja hapa kufanya maandalizi yetu ya mwisho ambayo yatatuwezesha sisi kuondoka na alama tatu licha ya kwamba tunacheza ugenini, lakini mpira hauna ugeni kikubwa ni kujipanga tu.

Desemba 19 mwaka huu, KMC FC ilicheza na Timu ya Ihefu katika uwanja wa Highland Estate Ubaruku, ambapo awali pia ilicheza na Simba katika uwanja wa Mkapa, Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro na hivyo kupoteza michezo yote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...