Mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa , Njombe, Lindi za Mtwara, Ruvuma pamoja na maeneo ya Kusini mwa Mkoa wa Morogoro..
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA iliyotolewa leo Desemba 25 2020 imeonesha kwamba leo Desemba 26 na 27 mvua kubwa itanyesha kwenye baadhi ya mikoa hiyo.
"Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo.
Aidha taarifa hiyo imetoa angalizo la kuwepo kwa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 Deaemba 28, mwaka huu.
Angalizo hilo limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, na Pwani ikijumuisha visiwa vya unguja na Pemba.
"Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuathirika kwa shughuli za uvuvi na ucheleweshwaji wa usafiri
Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Desemba 26 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Desemba 29, 2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...