***********************************************

Hali hiyo imebainika wakati Naibu waziri wa Ajira, Kazi na Vijana Mhe Patrobas Katambi alipofanya ziara kutembelea vikundi vya vijana vilivyokopeshwa vitendea kazi vinavyowasaidia katika shughuli zao za ujasiriamali.

Amesema kwa kumpatia kijana kifaa ni uamuzi mzuri unaomwepusha kutumia fedha kinyume na utaratibu na kumuondolea tamaa za matumizi mabovu hali inayompelekea kutokukamilisha malengo mahususi

“Niwapongeze pia kwa ajili ya eneo hili la utoaji mikopo, Kinondoni mmeweza kwa kuhakikisha mnasimamia taratibu, Sheria, kanuni na miongozo invyoelekeza kuhusiana na suala hili ngazi kwa ngazi kwani mchakato unaanzia ngazi ya chini hali inayopelekea kupata watu sahihi zaidi wa kuwapatia fedha hizi” Ameongeza Mhe Katambi

Akiwa Katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha EZEMA, Naibu waziri huyo ameridhishwa na bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo na kuahidi kuwa balozi wa bidhaa hizo popote atakapokwenda.

Aidha amewataka vijana wa kiume kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hii kwani takwimu za Sasa zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaojitokeza kuchukua mikopo ni kubwa zaidi ukilinganisha na vijana.

Awali akitoa Taarifa ya utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Kinondoni, Bi Halima Kahema amesema wameamua sasa kukopesha vifaa, na viwanda vidogo ili kuwawezesha wajasiriamali kwenda moja kwa moja kwenye uzalishaji.

Kadhalika amebainisha kuwa kwa mwaka 2017 wamefanikiwa kukopesha zaidi ya vikundi 5000 na kuwa kwa mwaka huu wa fedha wameshatoa mikopo kwa vikundi 202 ambapo wamepata kiasi cha shilingi Bil 1.3 .

Naibu waziri akiwa amembatana na Kamishna wa Kazi nchini ametembelea kikundi cha kutengeneza juisi cha Emitote na kikundi cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha EZEMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...