Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KATIKA kuhakikisha Sekta ya Uwekezaji nchini inaendelea kukua kwa kasi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo ameendelea na uhamasishaji katika kutangaza vivutio vya Uwekezaji kwa kutembelea Miradi mbalimbali Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Prof. Kitila ametembea Kiwanda cha KNAUF Gypsum Tanzania Limited cha uzalishaji ‘Gypsum’ kilichopo mkoani Pwani ambacho kinazalisha bidhaa mbalimbali za ‘Gypsum Boards’, ‘Metal Profile’ na ‘Plaster Powder’ mahususi kwa ujenzi.
Akizungumza wakati wa ziara yake Kiwandani hapo, Prof. Kitila amepongeza uwekezaji huo kwa Uwekezaji hilo bora katika eneo hilo la mkoa wa Pwani, amesema Serikali inahitaji uwekezaji ambao unazalisha Ajira kwa Vijana na kuheshimu utu wa Watanzania.
Prof. Kitila amepongeza Kiwanda hicho kukosa changamoto nyingi, pia ameeleza Serikali inahitaji kuwa na Uwekezaji ambao utaleta faida.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ilse Boshoff amesema wamevutiwa kuwekeza Tanzania kutokana na jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, hivyo wao kuona fursa ya Uwekezaji.
Pia ametembelea Kiwanda cha Bakheresa Group ambacho kinazalisha Unga kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam, Prof. Kitila amesema Serikali ina maono ya kuvutia, kuchochea Uwekezaji ili kusukuma Uchumi.
“Bakheresa ni Mwekezaji mkubwa hapa nchini, sisi tumekubali kwa hilo tunaona ametoa ajira kwa Watu wapatao 4500 ambao ni wengi. Pia ni Mwekezaji anayetumia Malighafi za hapa ndani Kwa hiyo ni Mwekezaji muhimu kwa Wakulima”, amesema Prof. Kitila.
Amesema kuna uhitaji mkubwa wa mazoa ya Kilimo hivyo ni budi kwa Wakulima wa ndani kuhakikisha wanakuzi Kilomo cha ndani ili kuwa na Malighafi za kutosha kwa Wawekezaji, pia amesisitiza kuwa na ushirika kwa Wakulima hao ili kufikia lengo la uzalishaji wa Malighafi hizo.
Katika Kituo cha Kipya cha Mabasi kilichopo Mbezi Luis, Prof Kitila amefika kuangalia fursa za Uwekezaji kwa Wawekezaji wa ndani na wa nje, ameagiza Kituo cha Uwekezaji TIC kufanya uchambuzi wa kutosha kuhusu fursa zinazopatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...