MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwakaribisha wananchi wote kwenye hafla ya ufungaji wa Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania itakayofanyika kesho tarehe 9 Desemba, 2020 kwenye ukumbi wa Saba Saba uliomo ndani ya Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K.Nyerere (al maarufu Sabasaba,) Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Hafla hiyo itaanza saa tano kamili asubuhi. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe Hemed Suleiman Abdulla Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Wote mnakaribishwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...