Mtafiti wa Mifugo Mwandamizi wa  Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) kituo cha Mpwapwa mkoani Dodoma  Mary Magonka, amewataka wafugaji wa kuku wa nyama kuacha utaratibu wa kuuza kuku wao kwa kukadiria, na badala yake wawauze kwa kupima kwa mzani.

Magonka aliyasema hayo wakati waandishi na watafiti walipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TaLIRI) wilayani Mpwapwa ,Dodoma

Amesema katika sehemu ambayo itafanya Wafugaji wa kuku kufurahia soko ni pale wanapouza kwa kuzingatia uzito na kuacha mazoea ya kuuza bila kuzingatia uzito hali ambayo inafanya ufugaji kuonekana mgumu kutokana na gharama za uendeshaji ufugaji huo.

“Wafugaji wa kuku wanauza kuku mmoja kwa bei ya kati ya sh. 8,000 hadi 10,000 kwa kukadiria, lakini kuku huyo huyo anaweza kuuzwa hadi 15,000  endapo atauzwa kwa kuzingatia uzito wake halisi,”amesema Magonka.

Magonka anasema katika utafiti uliiofanywa kwa kuhusisha kuku 157, umegundua ya kuwa endapo kuku dume/jogoo atapimwa urefu wake kwa kutumia futi, ataweza kukadiria uzito halisi, pia kuku jike atapimwa kwa upana wake pia ataweza kukadiria uzito wake halisi
mtafiti huyo anasema ya kuwa hii itasaidia wafugaji kupata njia mbadala ya bei rahisi ya kukadiria uzito halisi wa mifugo yao, badala ya mizani, ambayo ni gharama kubwa kwa wakulima kuweza kuwa nayo kila inapohitajika

“Serikali sasa iweke utaratibu wa kuuza kuku wa nyama kwa kupima kilo halisi ili wakuklima waache kunyonywa na madalali, bali wapate thamani sawa ya jasho lao ambapo itavutia zaidi ufugaji wa kuku nchini na watanzania wengi kujikwamua kimapato"amesema

Magonka aliongeza kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na kuku Zaidi ya milioni 80  na inaweza kuwa mchango muhimu kwenye uchumi wa taifa endepo mfugaji atawekewa mikakati halisi ya kupata mapato makubwa zaidi ya kazi yake.

Mkurugenzi wa taasisi cha utafiti wa mifugo (TALIRI) Mpwapwa Dk Haruna Chawala akizungumza na waandishi wa Habari na watafiti walitembelea Kituo cha Mpwapwa namna wanavyofanya Utafiti mbalimbali wa wanyama.

Kaimu mkurugenzi wa tume ya sayansi na Teknolojia (Costech) Dkt.Philbert Luhunga  akiangalia Mbuzi  wanaotafitiwa na kuboreshwa kisayansi katika eneo la Taasisi ya Mifugo na Kilimo TALIRI  wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi  wa Costech Dkt philbert  Luhunga akiangalia pamoja na waandishi wa Habari na watafiti wakiangalia namna chakula Cha mifugo kinavyoandaliwa wakati walipokwenda katika Kituo
Kuku aina chotara wakiwa katika kituo cha utafiti
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...