Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Furahika Education College, David Msuya katika ofisi ya Chuo cha Furahika Education College Jijini Dar es Salaam.
Msuya amesema katika Chuo chao wamekuwa wakitoa elimu ya Ufundi bure katika nyanja mbalimbali huku mzazi akitakiwa kuchangia Vifaa vya masomo pekee.
"Tunatoa elimu ya Ufundi bure kabisa, lakini mzazi atatakiwa kugharamia vifaa vya masomo, hatupokei fedha ya vifaa bali mzazi atatakiwa kufika navyo vifaa hivyo kama fomu inavyojieleza." Amesema Msuya.
Aidha amewataka wazazi kuwapa nafasi ya masomo watoto wa kike ili kuweza kuwaepusha na vishawishi na kukaa nyumbani kwani wao wanatoa elimu hiyo bure ikiwa dhamira yao kuu ni kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Vilevile katika fani ya ushonaji wamesema wamekuwa wakitoa zawadi kwa kila mhitimu pindi anapomaliza mafunzo, ambapo kila mhitimu hupewa Cherehani moja ili kwenda Kuanzia kazi yake ya ushonaji.
Pamoja na hayo amempongeza Rais Wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua yake ya jana ya kutokutekeleza adhabu ya kifo kwa baadhi ya wafungwa.
Kozi zinazotolewa na Chuo hicho amesema ni pamoja na Ufundi wa kushona, Elimu ya Kompyuta,Upambaji na ususi,Ufundi rangi,Ufundi bomba,Kilimo na kozi nyingine mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...