#Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa  China, Mhe. Wang Yi atafanya ziara hapa nchi Disemba, 7 na 8 mwaka huu.

#Ziara hii imekuja mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya simu kati ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Xi Jinping mnamo Disemba 15, 2020.

#Mhe. Waziri Yi akiwa hapa nchini atafanya shughuli zifuatazo; atakuwa na mazungumzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli pia atakuwa na mazungumzo rasmi kati yake na ujumbe wake pamoja na mimi na ujumbe kutoka Tanzania.

#Akiwa hapa nchini atazindua Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Wilaya ya Chato ambacho kimejengwa kwa fedha za watanzania ambapo Ukumbi mmoja umepewa jina lake.

#Sababu ya kumuomba afungue chuo hicho ni utamaduni wetu wa kumpa heshima mgeni, sambamba na kutambua elimu ya ufundi ilivyopiga hatua huko China.

#Aidha, Serikali ya China itajenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la  Serikali la kujenga Vyuo vya VETA kila Wilaya hapa nchini.

#Siku ya Ijumaa asubuhi Mhe. Waziri Yi atatembelea mwalo wa Chato ili kuona shughuli za uvuvi, ikizingatiwa kuwa ziwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani.

#Kati ya masuala ambayo Mawaziri wa Mambo ya Nje tutayazungumza ni pamoja na kupanua wigo wa biashara za Tanzania nchini China, kushiriki maonesho ya biashara ili kukuza bidhaa zetu pamoja uwekezaji katika sekta ya madini.

#Tutajadiliana pia kuhusu utoaji wa mikopo pamoja na uzalishaji wa umeme wa maji katika baadhi ya maeneo nchini.

#Nchi ya China imepiga hatua kubwa katika suala la teknololojia. Kuhusu utalii tunatarajia mwezi ujao kuanza safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es salaam hadi Guanzhou ili kukuza biashara na utalii. 

#Ziara hii imetusaidia pia kuwataarifu watu wa China kuhusu hifadhi mpya tano zilizofungulia hivi karibuni ikiwemo ya Burigi, Chato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...