Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo
amewataka wahitimu wa mafunzo ya askari wa akiba katika kijiji
cha Limamu wilayani humo kuilinda amani ya nchi yetu kwa kutoa
taarifa dhidi ya wahalifu au kuwakamata wahalifu wenye nia mbaya
na amani ya nchi yetu.
Kizigo amewataka kuwa askari wema wenye kufuata sheria za kazi
zao katika kuisaidia serikali huku akiwataka pia wasijiingize katika
kupokea rushwa katika kazi zao kwa kuwa rushwa ni adui Wa haki
katika jamii.
“Tunawategemea katika kuwakamata waweka mimba wanafunzi, hivyo
mkijihusisha na upokeaji rushwa mtasababisha kutowakamata wahalifu
na nafasi ya kazi yako haitakuwa na manufaa kwa jamii na hata kwa
serikali. “ alisema Kizigo.
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Limamu bi. Agnes Nchimbi alisema
kuwa vijana waliojiandikisha katika kujifunza Mgambo walikuwa 140
lakini kutokana na sababu zisizozuilika za kiafya vijana wengine
waliacha na kubakiwa na vijana 91 ndio waliohitimu mafunzo hayo
katika kijiji chake.
Pancras Newa mhitimu wa mafunzo hayo alisema walianza mafunzo
mwezi mei 2020 na kuhitimu mwezi januari 2021 hivyo aliiomba
serikali kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana wengine kwa kuwa
mafunzo hayo yanawafanya vijana wawe wakakamaVu , kuzijua mbinu
mbalimbali za kivita pamoja na kujua kutumia silaha alisema Newa.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Limamu bwana Magnus Ndunguru
alisema walihamasisha vijana kujiunga na Mgambo katika kijiji hicho
kupitia mikutano ya hadhara ya kijiji na kuwapata vijana 140
lakini kulingana na matatizo ya kiafya walibahatika kuhitimu ni hao
91.
Sherehe ya kuhitimu mafunzo ya jeshi la akiba katika kijiji cha
limamu yalifanyika katika uwanja wa shule ya msingi Tumaini
ambapo mkuu wa wilaya ya Namtumbo alipokea viapo vya askari wa
akiba hao pamoja na kukagua gwaride lililoandaliwa na askari hao wa
akiba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...