MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela chilumba, amewataka Wajasiriamali na wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa kufanya biashara halali, na kulipa kodi halali, pia kuacha kuingiza bidhaa kutoka nje ya Nchi na kukwepa kulipa kodi.
Ameyasema
hayo hivi karibuni, wakati akiongea na wafanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa
katika kikao cha kujadili mambo masuala ya biashara na maendeleo, kikao hicho
kilichofanyika Ukumbi wa Baylive uliopo Mbamba bay Wilayani humo.
Chilumba
amefafanua kuwa, wafanyabiashara na wajasiriamali wa Wilaya ya Nyasa
wanakabiliwa na changamoto ya ukwepaji ulipaji kodi, na kuingiza bidhaa
mbalimbali kutoka nje ya nchi hususani, Msumbiji na Malawi kwa njia za panya ili
kukwepa kulipa kodi halali ya Serikali, na kuikosesha nchi yetu Mapato ambayo yangeweza
kujenga miundombinu ya Nchi.
Aliongeza
kuwa amelazimika kuitisha kikao hicho, ili aweze kutoa elimu kwa
wafanyabiashara hao, ili waweze kupata elimu ya ulipaji kodi, na kutoa agizo la
kuacha mara moja tabia ya kuingiza kiholela kwa njia za magendo bidhaa
mbalimbali kama vile mafuta ya kupikia, yanayotoka Nchini Msumbiji na Sukari
inayotoka Nchi ya Malawi.
Aidha amewataka
wajasiriamali kufuata kanuni, taratibu
na sheria za kuingiza bidhaa hizo kutoka nje ya Nchi kwa kukata leseni.
“Tunachangamoto kubwa ya Wafanyabiashara wengi ya kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka Nchi ya Msumbiji na Malawi, hasa Sukari na Mafuta ya kupikia, ambayo huingia kwa njia isiyokuwa halali na kukwepa kulipa Kodi. Nichukue fursa hii kuwaambia kuwa majina ya wafanyabiashara hayo tunayo na tumekuwa tukikamata na kutaifisha pamoja na wahusika kuwachukulia hatua kali za kisheria, lakini bado wanaendelea kufanya biashara haramu.
Amesema kama Serikali wana wajibu wa kutoa elimu kwa
Wafanyabiashara, ili wafuate Taratibu kama tulivyoamua kuwaita kwa siku ya leo.
Ili Nchi ipate mapato ni Lazima Kila mfanyabiashara walipe kodi halali, na
tutahakikisha tunawachulia hatua za kisheria, wale wote watakaokwepa kulipa
Kodi ya Serikali.
Aidha
katika hatua nyingine amewapongeza wafanyabiashara hao kwa kuchangamkia fursa
za Kibiashara wilayani Nyasa kwa kuleta Bidhaa Mbalimbali na kuhakikisha kila
aina ya bidhaa inapatikana katika Wilaya ya Nyasa hususani katika Mji wa Mbamba
bay Ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Nyasa.
Kwa
upande wao wafanyabiashara Wilayani hapo, wameiomba Serikali ya Tanzania,
kupunguza ushuru na Tozo hasa katika Bidhaa za Nje kwa kuwa kinachosababisha
wakwepe kulipa kodi ni kiwango kikubwa cha tozo wanachotozwa na Mamlaka ya Kodi
Tanzania (TRA) hali inayowapelekea wafanyabiashara
hao kutopata faida.
Wameongeza
kuwa kama Serikali itaweka viwango rafiki vya ulipaji kodi ya Bidhaa
zinazoingia toka Nchi jirani itasaidia kufuata sheria kanuni na Taratibu za
ulipaji kodi.
Kwa
upande wake Afisa Biashara wa Wilaya ya Nyasa Zaitun Hamza, amewataka
wafanyabiashara hao kufahamu kuwa viwango vya
kodi wanazotozwa, ni kwa mujibu wa Sheria ya Kodi hivyo hakuna anayeweza
kupunguza viwango hivyo vya kodi. Aidha amewahamasisha wafanyabiashara hao
kununua na kuuza bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi ili kukuza uchumi wa Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...