MKUU wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein amewaasa wafanyakazi wa Chuo hicho kuwa wazalendo katika kukipaisha chuo ili waombaji wa elimu ya juu waweze kukikimbilia katika chuo hicho kikongwe ili kuendeleza taaluma zao.

Hayo ameyasema wakati wa kutambulishwa rasmi katika Ndaki ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipofika kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Januari 5, 2021. Amesema kuwa wafanyakazi kama hawatashirikiana hawatatimiza malengo ya Chuo.

"Na kazi yenyewe haiwezi kufanywa na mtu mmoja, kazi hufanywa na sisi sote kila mmoja kwa nafasi yake, kila mmoja kwa wadhifa wake, kila mmoja kufanya kile alichopangiwa kwahiyo ni kazi yetu sote na sisi tuchukue mpango wa kupigania elimu na ubora wake pamoja na kukipaisha chuo chetu ili kiwe bora zaidi na watu wakikimbilie zaidi." Amesema Dkt. Shein.

Hata hivyo amesisitiza uzalendo kwa wafanyakazi wote na kuwa na ushirikiano kwani mipango mingi iliyopangwa lazima itimie kwa kushirikiano ili kukisaidia chuo kikuu hicho kiweze kundelea.

"Nasisitiza umuhimu wa wafanyakazi kushirikiana kwa pamoja, katika lengo kuu la nchi yetu ni kuinua sasa Chuo Kikuu Mzumbe kwani Mzumbe tunakila kitu, kuna Baraza la chuo, mwenyekiti, katibu,Mzumbe tunaseneti, kunamajengo mapya kwahiyo lengo letu la kuleta maendeleo katika elimu. Litatimia hili tukishirikiana pamoja. Amesema Dkt.Shein."

Dkt. Shein amesema kuwa katika kuhakikisha elimu hapa nchini inakuwa bora zaidi lazima kuhakikisha maendeleo yanakuwepo katika kuboresha elimu zaidi ili kuwa na viongozi wenye maono yenye maendeleo kwa taifa letu.

Lakini Dkt. Shein amewaasa kuanzisha programu ambazo zinahitajika zaidi ili kutatua changamoto katika jamii.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka alimshukuru kwa kutembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kuahidi kushirikiana na mkuu na Dkt. Shein.

Hata hivyo amemuahidi kupokea ushauri atakaoutoa kwani anauzoefu mkubwa katika kuongoza vyuo vikuu hapa nchini.

Katika Ziara hiyo Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Shein amepata taarifa fupi ya maendeleo ya ndaki hiyo, alizungumza na wafanyakazi wa ndaki ya Dar es Salaa-Upanga na kisha kuelekea Kituo cha Tegeta ambapo alipata nafasi ya Kuzungumza na wanafuzi wanaosoma shahada ya kwanza pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu.

Miongoni mwa Viongozi alioambatana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakari Kunenge na Mkuu wa wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea ndaki ya Dar es Salaam kituo cha Tegeta.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akimwagilia mti mara baada ya kupanda katika viwanja vya Kituo cha Tegeta cha Ndaki ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe.Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na wafanyakazi wa Ndaki ya Dar es Salaam-Upanga ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Chuo Kikuu Mzumbe, Mhandisi Profesa Metthew Luhanga akizungumza na wafanyakazi wa chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakati wa Ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Lughano Kusiluka akizngumza na wafanyakazi wa Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipotembelea katika ndaki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakari Kunenge akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipotembelea kamapasi ya Dar es Salaam.
Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi akizungumza na wafanyakazi wa Ndaki ya Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Rose Joseph akizungumza wakati wa wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipotembelea Kamapasi ya Dar es Salaam Kituo cha Tegeta.

Picha za Pamoja.
Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe alipotemelea Ndaki ya Dar es Salaa kituo cha Tegeta.




    Matukio Mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...