Kaimu Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa mafunzo ya kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 wakati wa mkutano uliofanyika makao makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Januari 19, 2021, Mafunzo hayo yalipangwa kuanza hivi karibuni katika makambi mbalimbali ya JKT.
Na Mwandishi wetu Globu ya Jamii.
JESHI la kujenga Taifa (JKT) limesitisha mafunzo kwa kundi la kujitolea ya kwa mwaka wa mafunzo wa 2020/2021 yaliyotarajia kuanza hivi karibuni katika kambi malimbali hapa nchini kote.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena wakati akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino
mkoani Dodoma leo, amesema kuwa maafunzo hayo yaliyotarajiwa kuanza hivi karibuni yamesitishwa kwa muda mpaka hapo yatakapotangazwa.
"Kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti Makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa ajili ya kujitolea warejee majumbani kwao na wale ambao walikuwa bado hawajaripoti wasiende kuripoti kambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena." Amesema Kanali Mabena.
Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiwajengea vijana uwezo wa kujiajiri kupitia stadi za maisha wanazopata katika mafunzo yanayotolewa kwa mujibu wa sheria na yale ya vijana kujitolea, hivyo kuwawezesha kuwa wazalendo wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi waTaifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...