Jopo la wakaguzi kutoka Taasisi ya elimu ya vyuo vikuu nchini TCU likiongozwa na Prof John Kondoro  limefanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya maabara katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) inayotarajiwa kufundishia masomo ya uzamili ya masuala ya Nyuklia katika  Taasisi ya  sayansi  na teknolojia ya Mandela ya jijini Arusha.

Wakaguzi hao wamekagua maabara mbali mbali zilipo  makao makuu ya Tume hiyo iliyopo jijini Arusha na kufanya mazungumzo na  viongozi wa Tume  kwa ajili ya maandalizi ya masomo hayo yanayotarajiwa kuanza baadae mwaka huu.

Mkuu wa wataalamu hao Prof John Kondoro amesema wamejionea miundo mbinu hiyo na kwamba watakaa na watalaamu wengine kwa ajili ya kujadiliana  kwa kina kuhusiana na ukaguzi waliofanya.

Kwa upande wake, Afisa idhibati TCU, Bwana Aidan Mhonda amesema wamejionea maabara hizo za Tume ambapo wanaamini majadiliano yatakamilika na ripoti kutolewa kabla ya kuanza kufanyika kwa masomo hayo ambayo yataendeshwa kwa ushirikiano wa TAEC na Tasisi ya Mandela.

Naye Afisa mdhibiti ubora wa Taasisi ya  sayansi  na teknolojia ya Mandela bwana Otto Matonya amesema kuwa masomo hayo kwa hatua ya uzamili kwenye masuala ya nyuklia  yatasaidia katika kuzalisha watalaamu wengi wa teknolojia ya nuklia hapa nchini, hivyo wanaendelea kujipanga katika kuhakikisha  wanafanikiwa kwa kiwango kikubwa. Teknolojia ya nuklia ina mchango mkubwa  katika maendeleo ya nchi.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...