RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imedhamiria kuendeleza amani, umoja na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Zanzibar ambayo inakwenda  sambamba na misingi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere ukiongozwa na Mkurugenzi  wake Joseph Butiku uliofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kwua Rais wa Zanzibar pamoja na kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa  kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeweza kuimarisha amani, umoja na mshikamano hapa Zanzibar  hatua ambayo ni chachu ya maendeleo na imekuwa ikisisitizwa siku zote na Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Alisema kuwa hivi sasa kumekuwepo maelewano na mashirikiano makubwa kati ya viongozi pamoja na wananchi walio wengi wa Zanzibar hali ambayo imepelekea kuimarika kwa umoja, amani na mshikamano tokea kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hapa nchini.

Aliongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na maridhiano yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo lengo na madhumuni yake makubwa ni kuendeleza umoja, amani na mshikamano ili Zanzibar izidi kupata maendeleo na wananchi wake wazidi kuelewana.

RAIS wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mhe.Joseph Butiku, wakati alipofika Ikulu kwa mazungumzo na Ujumbe wake waliokaa (kulia ) mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.,Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa baadhi ya Vitabu vya historia ya Mwalimu Julius Nyerere na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere  Mhe.Joseph Butiku,  baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo,21-1-2021.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mhe. Joseph Butiku (kulia kwa Rais) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo leo 21-1-2021.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mhe. Joseph Butiku (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...