Magari 6 yaliyoshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kuibwa katika maeneo mbali mbali hapa nchini yakiwa kituo cha polisi mjini Njombe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akionyesha moja ya kifaa cha kutengenezea magari kilichokamtwa na mmoja wa watuhumiwa anachokituima kwa ajili ya ufunguaji wa nati ndani ya gari.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akionyesha aina ya magari wanayoshikilia na mahali yalikopatikana ili kuwasaidia wenye mali zao kuzitambua.


Na Amiri Kilagalila, Njombe

WATUHUMIWA  5 wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa magari 6 yaliyopatikana mikoa tofauti yanayosadikika yametokana na ujambazi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema wanashikilia gari 6 yaliyoibwa katika maeneo tofauti huku watuhumiwa 5 wakiendelee kuwahoji juu ya kuhusika na tuhuma za wizi huo.

“Tulikuwa tunatafuta gari moja matokeo yake tumeweza kukamata gari zingine 6 ambazo zinahusishwa na kuibwa maeneo mbali mbali katika nchi yetu.”Alisema Kamanda Issa.

Kamanda aewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na 

“Kuna mshtakiwa maarufu Endrick Husein jina maarufu (Kimya kimya) huyu ni mkazi wa Dar es salaam, Sudy Mwinyi mkazi wa Uyole Mbeya, Method Mkongwa mkazi wa Njombe, Iman Phidelis mkazi wa Moshi fundi magari pamoja na Timoth Nehemia mkazi wa Mufindi hawa wanashirikina kuiba magari na kuyapokea.”alisema Hamis Issa.

Amesema gari wanazoshikiria ni pamoja na aina ya Noah rangi ya silver iliyoibwa mkoani Mbeya,Gari aina ya Spacio iliyotoka Silali mkoani Mara,Rava 4 iliyokamatwa mkoani Singida,Carina iliyopatikna mjini Njombe.

Amewataka watanzania waliopotelewa na gari hizo kufika mkoani Njombe na vielelezo ili waweze kutambua gari zao kwa kuwa kwa sasa zipo mikononi mwa polisi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...