Wito
umetolewa kwa maafisa ugani mkoani Morogoro kufanya kazi kwa bidii ili
kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula hususani zao la Mahindi.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati wa
halfa ya kukabidhi pikipiki 10 zilizotolewa na Serikali ya China na
serikali ya Mkoa wa Morogoro kwa maafisa ugani 10 kati ya 42 waliofanya
vizuri katika utekelezaji wa Mradi wa kukuza kilimo cha zao la mahindi
mkoani Morogoro, mradi una
otekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha China na Serikali ya Mkoa wa Morogoro huku ukisimamiwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
otekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha China na Serikali ya Mkoa wa Morogoro huku ukisimamiwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Akizungumza
katika hafla hiyo, Sanare alisema kuwa mkoa wa Morogoro una ardhi kubwa
na nzuri ifaayo kwa kilimo cha mazao ya aina mbali mbali ikiwemo
mahindi lakini uzalishaji wa zao hilo uko chini kulinganisha na ubora wa
ardhi ya mkoa huo.
“
Mradi huu wa kukuza kilimo cha zao la mahindi, umeonesha tija na
ninatumai kuwa utakuwa na tija kubwaza zaidi katika kukuza uzalishaji wa
zao hili muhimu la chakula. Ni wakati sasa maafisa ugani kumuunga
mkono kwa vitendo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John
Pombe Magufuli, kuchapa kazi kwa bidii, kutoka ofisi na kwenda kwa
wakulima kuwafundisha njia bora za uzalishaji wa zao hili ili wazalishe
kwa wingi”
Sanare aliongeza kusema kuwa pikipiki
walizopewa maafisa ugani hao ziwe chachu ya kufanya kazi kwa bidii kwa
kuwafikia wakulima mashambani mwao na kuwapatia utaalamu wa kuzalisha
kwa tija. Aliwaasa maafisa ugani hao kutotumia pikipiki hizo kwa
shughuli binafsi kinyume na malengo yanayo tarajiwa ambayo ni kuwafikiwa
wakulima kwa wakati.
Akitoa taarifa ya mradi mradi
huo wa kukuza uzalishaji wa kilimo cha zao la mahindi, Mratibu wa
mradi, Ernest Mkongo, alisema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka
2013 katika vijiji viwili na baadae kufikia vijiji 10 huku ukiwa
umeonesha mafanikio makubwa.
“Mradi huu unatarajiwa
kufikia ukomo mwaka huu wa 2021, ambapo zaidi ya wakulima 2000
wamefikiwa moja kwa moja. Ni matarajio yetu kuwa idadi hiyo ya wakulima
itaongezeka kwa haraka kwani tunao wataalamu wa kutosha wenye nyezo za
kuweza kulifikia kundi kubwa zaidi la wakulima mkoani hapa.” Alisema
Mkongo.
Naye Afisa Ugani
wa kijiji cha Mtego wa Simba,Halmashauli ya Morogoro, moja ya kijiji
kinachotekeleza mradi huo Veronica Lugano, alisema kuwa kabla ya mradi
huo wakulima walikuwa katika kijiji chake wakizalisha kati ya gunia 2
mpaka 3 kwa hekali moja, kwa sasa wakulima hao wanazalisha kati ya gunia
10 mpaka 20 kwa hekali moja.
Lugano alisema kuwa
ana matumaini makubwa kuwa tenkolojia hiyo ya kukuza uzalishaji wa zao
la mahindi ikiwa itatumiwa vizuri na wakulima itaufanya mkoa wa Morogoro
kuzalishaji zao la mahindi kwa wingi.
Alisema
kuwa maafisa ugani wamejipanga kusimamia kikamilifu uzalishaji wa zao
hilo mkoani Morogoro kwa kuhamasisha na kuwafundisha wakulima kulima
kilimo cha kisasa kwa kutumia kanuni bora za kilimo ili kuongeza
uzalishaji wa zao hilo kwa ajili ya kukuza uchumi wa mkoa wa Morogoro na
Taifa kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...