Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile (katikati) akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa kupeleka mawasiliano vijijini baina ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba (kushoto) na Mmoja wa wawakilishi wa mtandao wa simu.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya kupeleka mawasiliano vijijini awamu ya tano.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF, Justina Mashiba akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano baina ya mfuko huo na makampuni ya simu kupeleka mawasiliano vijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Zainab Chaula akizungumza kwenye hafla hiyo.


Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imeshuhudia utiaji saini wa mikataba ya kupeleka mawasiliano vijijini awamu ya tano baina ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF)  na makampuni ya simu za mkononi.

Hafla hiyo ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika jijini Dodoma leo na kushuhudiwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile.

Akizungumzia makubaliano hayo Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema katika mradi wa Mawasiliano Vijijini awamu ya tano jumla ya kata 61 zenye vijijini 173 na wakazi 728,840 zitafikishiwa mawasiliano huku alisema kwa mujibu wa mkataba huo hadi kufikia Oktoba mwaka huu mradi unatakiwa uwe umekamilika.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Faustine Ndugulile ameyaonya makampuni ya simu za mkononi juu ya utoaji wa siri za wateja huku akisema kuwa kwa kampuni itakayotolewa malalamiko ya kufanya hivyo itachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema Wizara hiyo itahakikisha inatunga sheria ya kuwalinda wateja wa simu za mkononi ili kuondoa tabia hiyo ya kutoa siri zao.

" Niwaonye makampuni yanayotoa taarifa za siri za wateja, tutawachukulia hatua wote kwa sababu kufanya hivyo ni kinyume na sheria hivyo kampuni itakayobainika itachukuliwa hatua.

Niyatake makampuni ya mawasiliano kusoma sheria na kuielewa ili waweze kufanya kazi kwa mujibu wa sheria. Lazima tuhakikishe tunapeleka mawasiliano huko maeneo ya mipakani badala ya kufikiria miji ya kibiashara tu,lakini pia tunapokuwa katika maeneo hayo tukaribishwe na mitandao ya kwetu na siyo ya nchi jirani," Amesema Naibu Waziri Dk Ndugulile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...