Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

VITA ilitangazwa jijini Dar e Salaam na Simba SC iliyopewa jina la kimombo ya WAR IN DAR (WIDA) rasmi imewaondoa FC Platinum baada ya kupokea kichapo cha bao 4-0 katika dimba la Benjamin Mkapa na kufanya jumla ya mabao 4-1.

Simba SC baada ya kumaliza Vita hiyo iliyotangazwa kwa kipindi cha muda mrefu na kupewa Jina la WIDA sasa inafuzu hatua ya Makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa mara ya pili sasa ikiwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

Wakiwa nyumbani katika dimba hilo la Kumbukumbu ya Mzee Mkapa, Simba SC kama kawaida yao walianza kutoa kichapo hicho cha bao 4 kupitia Beki wake, Erasto Nyoni kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 39 baada ya Shomari Kapombe kuchezewa faulo katika eneo la hatari.

Akiwa katika kiwango bora, Beki wa pembeni Shomari Kapombe alipachika bao la pili katika mchezo huo baada ya Golikipa wa Platinum kutema shuti kali la Kiungo Rally Bwalya, kazi haikuishia hapo, Mshambuliaji John Bocco aliiandikia Simba SC bao la tatu katika dakika za 90+1 baada ya kutengenezewa pasi safi na Rally Bwalya aliyekuwa kwenye kiwango bora katika vita hiyo.

Kiungo Maestro, Clatous Chota Chama, hakuwaacha salama FC Platinum baada ya kufunga ukurasa wa mabao kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 90+5, hiyo ikiwa baada ya yeye mwenyewe kuchezewa faulo katika eneo la hatari wakati akienda kusalimiana na Golikipa.

Licha kuwa na Staa wao, Perfect Chimwende aliyewafunga Simba SC mjini Harare, Zimbabwe, FC Platinum walizidiwa mbinu zaidi kipindi cha kwanza sambamba na dakika za lala salama za mchezo huo.

Simba SC sasa wamefuzu Makundi ya Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyofanya msimu wa 2018-2019 wa Michuano hiyo inayoshirikisha vigogo wa Soka barani Afrika.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...