Mratibu wa mradi wa kuwasaidia wajasiriamali katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania,  Safari Fungo, akifafajua jambo kwa wanahabari baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa Taasisi mbali mbali zinazosaidia wajasiliamali katika kuwajengea uwezo wa na kuongeza thamani kwenye bidhaa zao.
Mratibu wa mradi wa kuwasaidia wajasiriamali katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania,  Safari Fungo, akizungumza wakati akifungua  warsha ya siku mbili kwa Taasisi mbali mbali zinazosaidia wajasiliamali katika kuwajengea uwezo wa na kuongeza thamani kwenye bidhaa zao. Kushoto kwake ni Mkufunzi, Melkiado January.
Joan Mangawe, Afisa Mkufunzi Mwandamizi wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) akizungumza katika warsha hiyo.
Mkufunzi wa mafunzo ya wa kuwajengea uwezo wajasiliamali Melkiado January  akizungunza na wanahabari baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa Taasisi mbali mbali zinazosaidia wajasiriamali katika kuwajengea uwezo wa na kuongeza thamani kwenye bidhaa zao.
Mfanyakazi wa Wizara ya biashara na Viwanda katika wakala wa Viwanda vidogovidogo na vya kati Zanzibar Masoud Suleiman, akieleza namna mafunzimo hayo yatakavyowainua wajasiriamali wa Zanzibar na kuwawezesha kupata masoko.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wa warsha ya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja


KITUO cha biashara za Kimataifa Tanzania (ITC) kimedhamilia kuwakomboa wajasiriamali wa biashara ya Kahawa, Chai, viungo na Parachichi kwa kwa kuwajengea uwezo wa namna ya kutengeneza vifungashio bora ili wa waweze kukubalika na kupata masoko mengi.

Mratibu wa mradi wa Markup, wa kuwasaidia wajasiriamali katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Safari Fungo ameyasema hayo leo Januari 18,2020 wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa Taasisi za Umma mbali mbali zinazosaidia wajasiliamali mafunzo ya kuwajengea uwezo katika nyanja ya kuongeza thamani kwenye bidhaa zao na kupata masoko.

"Tuko hapa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajasiriamali pamoja na Taasisi za Umma ambazo zitajihusisha Katika masuala ya Vifungashio ili kuweze  kujua namna ya kuboresha bidhaa zao hususani kwenye eneo la vifungashio" amesema Fungo.

Amesema mafunzo hayo ya siku mbili, hayataishia hapo tu, wanufaika  wataendela kushikwa mkono na wataalamu kwa muda wa miezi mitatu hadi sita mpaka pale watakapokuwa wameweza kujisimamia kwenye bidhaa zao.

Mradi huu unawasaidia wajasiriamali waweze kuongeza thamani katika mazao hayo ili waweze kupata masoko kwa kuboresha vifungashio na kuweza kupata masoko, unapokuwa na kifungashio kizuri basi ni rahisi hata kipata masoko. Mfano unapoenda dukani ama sokoni kununua kitu chochote unachokiona kwanza kabla  kuifikia bidhaa ni  kifungashio  hivyo vifungashio na chapa ni eneo muhimu.  Baadhi wameishapata hi huduma hiyo  hii ni awamu ya pili, awamu ya kwanza tuliwajengea uwezo wajasiriamali wa chai.

Kwa upande wake Joan Mangawe, Afisa Mkufunzi Mwandamizi wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) amesema kama shirika wamekuwa wakiwasaidia wajasiriamali haswa katika eneo hilo la vifungashio ili kuhakikisha wanapoingia sikoni basi bidhaa zao zinakuwq kwenye ubora unaotakiwa kwa chapa na usindikaji.

 Amesema mafunzo hayo kutoka TIC ni  fursa nyingine ya kusaidia wajasiliamali kujua namna na kuweka chapa kufunga bidhaa zao vizuri ili waweze kupata masoko ya ndani na ya nje na waweze kupata faida kutokana na kile wanachokizalisha.

"Tutakapomaliza mafunzo haya tutakuwa na fursa zaidi ya kuwafundisha zaidi wajasiriamali namna bora ya kufungasha bidhaa zao na namna bora ya kupata vifungashio vilivvyo bora na ufungashaji unaokidhi matakwa ya viwango vilivyopo hapa nchini na nje ya nchi ili bidhaa zao ziweze kupata soko zuri" amesema Joan.

Ameongeza kuwa kwa upande wa wasindikaji wadogo wa kahawa ambao mafunzo hayo yanawalenga zaidi watapata nafasi ya kujifunza zaidi na kuelewa mahitaji ya soko yakoje kwani wakielewa watakuwa katika nafasi nzuri ya kuelewa nini kinatakiwa sokoni.

Amesema, pamoja na kufundisha masuala ya uzalishaji ulio bora na kuzalisha bidhaa bora lakini pia kuzingatia kifungashio vyenye viwango husika.

Naye, mkufufunzi wa mafunzo hayo na mshauri wa biashara upande wa vifungashio  Melkiado January amesema anawasaidia wajasiliamali katika sekta ya kahawa.  

Amesema, pamoja na mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wajasiliamali hao pia amekuwa akikutana na changamoto mbali mbali katika kutoa mafunzo ikiwemo namna ya kubadirisha yale wanayoyafundisha kwenda kwenye vitendo na pia wajasiliamali wamekuwa  wakikwama kujifunza haswa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha ili kuweza kubadirika moja kwa moja kwani baada ya kumaliza kujifunza juu ya vifungashio anatakiwa kwenda kuwekeza fedha akili na muda.

Kwa upande wake, muwakilishi kutoka Zanzibar Masoud Suleiman, ambaye ni mfanyakazi wa Wizara ya biashara na viwanda katika wa wakala wa viwanda vidogo vidogo  na vya kati Zanzibar amesema, mafunzo hayo ya ITC juu ya kutambua namna ya kutengeneza vifungashio yatasaidia pia kwenda kuwakuza wajasiliamali wanzibar na ili waje kupata masoko mazuri, wajasiliamali ni wengi wanazalisha  bidhaa nyingi isipokuwa tu hawana uelewa wa vifungashio na kufanya suala la masoko kuwa na Changamoto.

Biashara yoyote ikiwa na vifungashio vizuri soko linakuja lenyewe...tunaimani baada ya mafunzo haya wajasiriamali wazanzibar watanufaika kwa kuanza kuuza bidhaa zao kwa a kutukia vifungashio bora hasa katika kipindi hiki ambapo Serikali ya zanzibar inampango wa kujenga kiwanda cha vifungashio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...