Watuhumiwa wa biashara ya Dawa za kulevya wakiwa mbele ya waandishi wa habari( hawapo pichani) wakiwa katika Ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya .Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Heroine na Bangi jijini Dar es Salaam.
Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 27,2021 jijini Dar es Salaam kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa watatu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WATU watatu jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya baada ya kukutwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa ni aina ya Heroine gramu 400 pamoja na majani makavu ya bangi puli moja ambazo ni  sawa na kete 30.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamishna Generali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji amewataja watuhumiwa hao ni  Anadhati Rashid Mchongezi (20) Emmanuel Msakuzi(23) na Kulwa Sham as (49) maarufu mama Udodi ambaye pia ni Balozi wa nyumba 50 katika mtaa wa Juwaje Kunduchi Pwani.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Januari 22,mwaka huu katika eneo la Kunduchi Pwani Kauzeni wakiwa na dawa hizo na watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Amefafanua kuwa maofisa wa Mamlaka hiyo  baada ya kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata kiasi cha dawa hizo zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa nailoni.

"Mamlaka inaendelea kuwashikilia watuhumiwa na watafikishwa Mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika, tunaomba jamii kushirikiana na Mamlaka katika kukabiliana na dawa za kulevya, katika hawa watuhumiwa ambao tunawashikilia yumo kijana wa miaka 20, unaweza kuona kazi iliyopo mbele yetu katika kukomesha biashara ya dawa za kulevya.

"Tumejipanga na tutaendelea kufuatilia wale wote wanaojihusisha na biashara hii haramu ya dawa za kulevya,tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.Hakuna atakayeachwa ,tutawakama tu na katika hilo hatuna mzaha,"amesema Kamishna Generali.

Aidha amesema katika kipindi cha Novemba mpaka Desemba 2020 Mamlaka imefanikiwa kushinda kesi kubwa tatu ikiwemo iliyokuwa ikimhusisha mfanyabiashara maarufu wa jijini Tanga Yanga Omari Yanga maarufu Rais wa Tanga aliyehukumiwa  kifungo cha miaka 30 jela ."Mfanyabiashara huyo alikutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina Heroine zenye uzito wa gramu 1052.63 .

"Pia Mahakama Kuu ilimtia hatiani Ayubu Mfaume Kiboko na mkewe ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa gramu 251.25."

Ameongeza kuwa katika kupambana na kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya, Mamlaka ilifanikiwa kuwakamata raia wawili wa Irani waliotiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa gramu 111.02 waliomatwa katika Bahari ya Hindi ambao walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela pamoja na kutaifishwa kwa  Jahazi  lao ambalo walikuwa wakitumia kusafirisha dawa hizo.

Pia katika kipindi hicho Mamlaka imefanya operesheni mbalimbali na kufanikiwa kumkamata Kibinda Mohamed Selemani akiwa na dawa za kulevya aina ya Heroine kiasi cha gramu 135.12 na mtuhumiwa ameshafikishwa Mahakamani .

Kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na Mamlaka hiyo ,Kamishna Generali Kaji amesema katika kipindi cha mwaka 2020 Mamlaka imefanikiwa kufungua vituo vya kutolea tiba ya Methodone katika mikoa mbalimbali na siku za karibuni watafungua kituo cha tiba mkoani Arusha.Pia kuna.mikoa ya Mbeya, Pwani, Tanga, Dodoma na Mwanza.

Aidha kwa Dar es Salaam wameongeza vituo hivyo vya kutoa tiba maeneo ya Segerea, Mbagala  Rangi Tatu na Tegeta ambavyo vinavyotarajia kuaza kutoa huduma hiyo mwezi ujao na kuifanya Dar es Salaam kuwa na jumla ya vituo sita kati ya tisa vinavyotoa tiba ya Methodone nchini ili kupunguza msongamano uliokuwa katika vituo vitatu vya awali."Jumla ya waraibu 9500 nchini wamepata huduma kupitia vituo hivyo."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...