Mkuu wa kanda ya mashariki wa Mabalozi wa usalama barabarani Augustino Mkumbo akizungumza na mabalozi katika semina elekezi iliyofanyika katika ukumbi wa polisi kibaha mail moja mkoa wa Pwani
Mkuu wa kanda ya Kusini wa Mabalozi wa usalama barabarani Nassor Mansoor akizungumza na mabalozi katika semina elekezi iliyofanyika katika ukumbi wa polisi kibaha mail moja mkoa wa Pwani
Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Dar es salaam Mali Nicolus akionyesha moja ya dumu ambalo lilikuwa linatumika kama kiti ndani ya mojawapo ya basi mara baada ya kufanyiwa ukaguzi na askari wa kikosi cha usalama barabarani kwa kusirikiana na RSA
Salha Msonga Katibu wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa kanda ya mashariki wa Mabalozi wa usalama barabarani Augustino Mkumbo akizungumza na mabalozi katika semina elekezi iliyofanyika katika ukumbi wa polisi kibaha mail moja mkoa wa Pwani
Balozi wa Usalama barabarani Slim Yussufu akimsaidia mmoja wa abairia namna ya kufunga mkanda kwaajili ya usalama wake akiwa safarini
Balozi Paschal Makomba akijaribu kumpatia elimu kondakta wa basi aliyepatiwa cheti baada ya gari lake kukutwa na makosa jana katika stendi ya mabasi mail moja kibaha mkoa wa Pwani
Baadhi ya abiria kama wanavyoonekana katika picha wakipatiwa elimu ya usalama barabarani sambamba na kutakumbushwa wajibu wao wawapo safarini
Hali ilivyokuwa katika stendi ya mabasi ya Maili moja Kibaha mkoa wa Pwani
Pichani ni baadhinya abiria waliokuwa wakiomba kutatuliwa changamoto iliyojitokeza mara baada ya kukaa muda mrefu bila dereva na kondakta kulipa deni lililokuwa likidaiwa katika gari hilo jambo amabalo liliwaletea usumbufu
Baadhi ya mabalozi wa Usalama barabarani wakiwa katika semina elekezi iliyofanyika katika ukimbi wa polisi kibaha mail moja mkoa wa Pwani
Na.Vero Ignatus,Pwani
Ni wajibu wa abiria kutokukaa kimya na wanao wajibu wa kupaza sauti zao pindi wanapoona vyombo vya usafiri vinahatarisha usalama wa Maisha yao
Hayo yanesemwa na mkuu wa kanda ya mashariki wa mabolozi wa usalama barabrani (RSA )Augustino Mkumbo katika stendi kuu yam abasi Kibaha mkoa wa Pwani katika mwendelezo wa kampeni ya 'Abiria Paza Sauti' lengo likiwa kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani.
Katika zoezi hilo mabalozi hao walishirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa pwani,ambapo zaidi ya magari 40 yalikaguliwa, na badhi ya magari yaligundulika kuwa na makosa mbalimbali, ikiwemo abiria kukalia madumu ya maji,vigoda na vistuli na huku gari nyingi zikiwa hazina mikanda.
Kwa upande wake mmoja wa abiria wa gari ya Luwinzo kutoka ubungo kwenda Makambako alisema kuwa changamoto waliyokumbana nayo ni pale dereva gari yake inadaiwa na anashindwa kulipa kwa wakati inaleta usumbufu sana kwetu abiria
‘’Gari yetu ilitakiwa kutoka saa kumi na mbili asubuhi,kutoka mbezi kuelekea Makambako hadi sasa nne asubuhi hatujaondoka ana anashidnewa kulipa deni kwa wakati anzia asubuhi tumekaa karibia saa moja’’ alisema abiria
Kwa upande wake mmoja wa balozi Leyla Banji aliweza kutoa wito kwa abiria kutokukubali kula chakula cha kupewa ndani ya gari kwa mtu wasiyemfahamu kwani inaweza kuwa hatari kwao nahata kuibiwa pale wanaposinzia n ahata kushushwa vituo ambavyo sivyo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mabalozi wa Usalama barabrani mkoa wa Dar es salaam Mali Nicolaus amesema kuwa ipo haja ya Mamlaka husika kutoa elimu kila mara kwa abiria, ili waweze kutambua usalama wake,hivyo wanatakiwa wabadilike na watambue thamani yao, kwani wanapolipa nauli wanatakiwa wapate huduma stahiki.
Sambamba na hayo kulikuwa na semina elekezi kwa mabalozi wa zaidi ya 25, iliyofanyika katika ukumbi wa polisi kibaha mail moja, ikiwa ni pamoja na kupitia na kuchambua kanuni za RSA. Njia sahihi, matumizi sahihi ya lugha wakati wa kuripoti,wajibu wa balozi pamoja na mambo ya kuzingatia kwa mabalozi wakati wa kutoa elimu kwa wahusika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...