MTEGO uliowekwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Kusini umefanikiwa kumnasa Jamaly Sad akiuza dawa za Serikali.
Taarifa ya TMDA inaeleza kwamba Sad amenaswa kwenye mtego huo Januari 31 ,2021 wilayani Newala na alikuwa akiuza dawa za Serikali za Mpango wa Uzazi.
Dawa hizo ni Medroxy Progesterone (vichupa 60) na Microgynon pills (vidonge 3360) zote zikiwa na thamani ya Sh. 300,000.
Hivyo kwa sasa Sad na mtoto wake wanatuhumiwa kuuza dawa hizo za Serikali na wamefunguliwa jalada polisi RB No.NL/RB/94/221 na yuko ndani kwa hatua zaidi kisheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...