SERIKALI inawaalika wabunifu kushiriki katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia (MAKISATU) ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi machi mwaka huu jijini Dodoma.
Akizungumza na Wandishi wa Habari jijini Dodoma leo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo amesema lengo la mashindano hayo ni kuibua, kutambua, kuadhimisha, kujenga, kukuza na kuendeleza ubunifu wa Watanzania katika nyanja za Sayansi na Teknolojia ili kuchangia juhudi za maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
“Matokeo tarajiwa ya MAKISATU ni kukua kwa hamasa ya ubunifu katika nyanja ya sayansi na teknolojia, matumizi ya sayansi, teknolojia, na ubunifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii; kuendeleza ubunifu ili kufikia hatua ya ubiasharishaji kuchochea ugunduzi na ubunifu wa kisayansi na teknolojia," Amesema.
Katibu mkuu amesema maonyesho ya MAKISATU tangu kuanzishwa kwake yamekuwa na matokeo chanya katika jamii kwa kuibua vipaji ambavyo vilikuwa vimejificha.
Amesema katika maonyesho ya mwaka 2020 zaidi ya wataalamu 1066 wameibuliwa na kuajiliwa na serikali sehemu mbalimbali na wengine kuendelezwa taaluma zao.
“Maonyesho haya yamekuwa na manufaa kwa serikali na jamii kwa ujumla kwani nchi yetu sasa imeingia katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo hatuna budi kuwaendeleza wataalamu wa ndani ambao ndio chachu kubwa ya maendeleo ya viwanda," Amesema.
Kwa upande wake Mkuerugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk Amos Nungu amesema Wabunifu watawasilisha maombi ya ushiriki kupitia kwa Taasisi zinazohusika na uratibu wa kundi.
Ameongeza kuwa waratibu wa kila kundi watafanya tathmini ya mawasilisho na kuchagua wabunifu kumi bora (10) kwa kila kundi ambao watashiriki kwenye fainali ya Kitaifa.
“Majaji watafanya tathmini ya kina kwa kila ubunifu katika hatua ya fainali kwa kupitia mawasilisho, kufanya mahojiano na mbunifu na kutathmini ubunifu, kisha utafanyika ulinganifu wa alama na kupata ubunifu mahiri tatu (3) kwa kila kundi utakao toa tuzo,"Amesema.
Dk Nungu amesema serikali itaendelea kutoa motisha kwa wadau na washiriki wa maonyesho hayo kwa kutoa zawadi mbalimbali ambazo zitaongeza chachu kwa washiriki.
Amezitaja zawadi za mwaka huu kuwa ni fedha taslimu na wataalamu kuchukuliwa na kwenda kuendelezwa taaluma zao katika maeneo mbalimbali.
Kauli mbiu ya MAKISATU kwa mwaka 2021 ni ”Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Endelevu”.
Home
HABARI
SERIKALI YAWAALIKA WABUNIFU KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAKISATU YATAKAYOANZA MACHI MWAKA HUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...