JUMUIYA ya Wanafunzi  wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania TAHLISO, wametembelea Bunge la 12  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma na kupata mafunzo mbalimbali ya uongozi na kujua namna bunge linavyoendesha shughuli zake.

Katika Ziara hiyo, TAHLISO iliyokuwa ikiongozwa na kamati kuu tendaji yake chini ya mweyekiti wake, Peter Niboye pamoja na Marais wa vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu na Elimu ya Kati Tanzania walipata pia 

Nafasi ya Kutembelea Ofisi ya TAHLISO inayojengwa Iyumbu Dodoma na kujionea namna ujenzi wa ofisi hiyo ya kisasa unavyoendelea kwa kasi ambapo kwa Sasa Ujenzi huo upo katika hatua za awali.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Niboye aliongoza usombaji tofali na uchanganyaji Saruji kwa ajili ya ujenzi  kwa kamati kuu tendaji TAHLISO na Marais wa vyuo ikiwa ni ishara ya Kuunga mkono zoezi hilo la ujenzi linaloendelea Jijini Dodoma.

Aidha Niboye amewaomba wadau mbalimbali wapenda maendeleo kujitokeza na kuunga mkono na kusaidia kufanikisha ujenzi huo unaoendelea ili kutimiza kiu na shauku ya  wanafunzi wa elimu ya juu na elimu ya Kati.

Kamati kuu Tendaji ya TAHLISO na Baadhi ya Marais wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma.
Kamati kuu Tendaji ya TAHLISO na Baadhi ya Marais wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali Tanzania wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge Dodoma.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Nchini (TAHLISO)  Peter Niboye akimsikiliza Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma.
Kamati Kuu Tendaji ya Jumuiya ya wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), marais wa Serikali ya wanadunzi kutoka vyuo mbali mbali nchini, wakiwa kwenye picha ya pamoja katika eneo la Iyumbu Dodoma mahali ambapo ofisi ya ya TAHLISO inajengwa.
Kamati Kuu Tendaji ya Jumuiya ya wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Dr. Leckton Moris akisogeza tofali kwenye ujenzi wa ofisi ya jumuiya hiyo, unaoendelea jijini Dodoma.
Kamati Kuu Tendaji ya Jumuiya ya wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Dr. Leckton Moris akisogeza tofali kwenye ujenzi wa ofisi ya jumuiya hiyo, unaoendelea jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...